Watoto 80,000 waliorejea DRC toka Angola wanahitahi msaada haraka:UNICEF

Wanawake na watoto wakiwasilia katika kituyo cha mpaka cha Chissand,Lunda Norte, Angola wakikimbia mashambulio ya wanamgambo katika mkoa wa Kasai DRC.2May 2017
© UNHCR/Pumla Rulashe
Wanawake na watoto wakiwasilia katika kituyo cha mpaka cha Chissand,Lunda Norte, Angola wakikimbia mashambulio ya wanamgambo katika mkoa wa Kasai DRC.2May 2017

Watoto 80,000 waliorejea DRC toka Angola wanahitahi msaada haraka:UNICEF

Amani na Usalama

Takribani watoto 80,000 waliorejea hivi karibuni nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kutoka Angola hivi sasa wanahitaji haraka msaada wa kibinadamu limesema shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF. 

Kwa mujibu wa taarifa ya UNICEF iliyotolewa leo zaidi ya raia 300,000 wa DRC wamerejea nyumbani tangu tarehe mosi Oktoba , hali inayozusha hofu miongoni mwa wadau wa misaada ya kibinadamu kwamba taifa hilo ambalo limeghubikwa na machafuko sasa liko katika hatihati ya zahma nyingine.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Geneva Uswis msemaji wa UNICEF Christopher Boulierac watoto waliorejea DRC hali yao ni tete

(SAUTI YA CHRISTOPHER BOULIERAC )

“Maelfu ya watoto wanatembea mwendo mrefu , wakikabiliwa na hali mbaya ya hewa , njaa, kutokuwepo usalama na hatari ya kufanyiwa ukatili. Wana fursa ndogo ya kupata maji safi na huduma za afya na pia wanakosa elimu. Tuna wasiwasi sana kuhusu hali zao n aza familia zao.”

Ameongeza kana kwamba hiyo haitoshi bei za vyakula zimeongezeka kwa kiasi kikubwa sana katika baadhi ya maebneo na kufanya hali kuwa mbaya kwa watoto hao na familia zao.

UNICEF na wadau wake wamefanya tathimini  ya mahitaji ya kibinadamu katika majimbo ya Kamako na Kasai ambako wengi wanaorejea ndio wanaishi na wanajiandaa kuwasaidia watoto na familia zao kwa kuwawekea mabomba ya maji safi ya kunywa, makazi ya dharura 27, kuwagawaia vyandarua vya mbu kuzuia malaria, kukabiliana na utapia mlo, kutoa chanjo za surua , kuwawekea maeneo ya kusomea na kuunganisha watoto na familia zao. Na kuweza kukidhi mahitajoi hayo UNICEF inahitaji dola milioni 3.