CERF yatoa dola milioni 3.5 kusaidia uhakika wa chakula Burundi
Mkuu wa masuala ya kibinadamu na misaada ya dharura wa Umoja wa Mataifa Martin Griffiths, leo ametangaza kutenga dola milioni 3.5 kutoka mfuko mkuu wa dharura wa Umoja wa Mataifa (CERF) ili kusaidia zaidi ya watu 38,000 walioathiriwa na uhaba wa chakula nchini Burundi.