Ukosefu wa msaada waongeza kiwewe kwa wakimbizi na wahamiaji watoto waliotimiza umri wa utu uzima Italia- Ripoti
Takribani wakimbizi na wahamiaji watoto 60,000 waliowasili nchini Italia bila wazazi ama walezi kati yam waka 2014 na 2018 ambao sasa wametimiza umri wa miaka 18 wanahitaji msaada endelevu ili waweze kumudu kipindi cha mpito cha kuwa watu wazima.