Ukurasa huu unaleta pamoja taarifa kuhusu muongozo kutoka kwa Shirika la afya la Umoja wa Mataifa, WHO na Umoja wa Mataifa kuhusu mlipuko wa sasa wa virusi vya corona au COVID-19, ambavyo viliripotiwa mara ya kwanza Wuhan, China mnamo Desemba 31, 2019. Tafadhali tembelea ukurasa huu kupata taarifa za kila siku. WHO inafanya kazi kwa karibu na wataalam wa kimataifa, serikali na wadau kupanua ujuzi wa kisayansi kuhusu virusi hivi vipya, kutokana na jinsi vinavyosambaa na athari zake na kutoa ushauri kwa nchi na watu, kuhusu hatua za kuchukua kwa ajili ya kulinda afya na kuzuia kuenea kwa mlipuko.
Taarifa kuhusu Virusi vya Corona
Ndege ya kwanza ya UN iliyosheheni msaada wa COVID-19 kuondoka leo kuelekea nchi za Afrika:WHO/WFP/AU
Ndege ya kwanza ya mshikamano ya Umoja wa Mataifa inatarajiwa kuondoka leo mjini Addis Ababa Ethiopia kuelekea nchi mbalimbali za Afrika ikiwa imesheheni msaada na vifaa ya kukabiliana na mlipuko wa virusi vya Corona au COVID-19.
Kutokana na ongezeko la COVID-19, zaidi ya watoto milioni 117 wako hatarini kukosa chanjo ya surua
Kutokana na taarifa iliyotolewa hii leo mjini Atlanta na New York Marekani, pamoja na Geneva Uswisi, wakati COVID-19 ikizidi kusambaa duniani, zaidi ya watoto milioni 117 katika nchi 37 wanaweza kukosa kupokea chanjo ya kuokoa maisha dhidi ya surua.
Mikakati ya kudhibiti COVID-19 inatofautiana; WHO yatoa mwongozo wa kufuata
Shirika la afya la Umoja wa Mataifa, WHO, kesho litachapisha mwongozo wenye taarifa zaid za kuwezesha nchi kuchukua hatua za kupunguza kuenea kwa ugonjwa wa virusi vya Corona, COVID-19 sambamba na kuwa msingi wa kuamua iwapo kurejesha shughuli za kiuchumi na kijamii au la.
Kijana mtanzania avumbua kifaa kinachoweza kusambaza elimu mahali pasipo na walimu
Ombeni Sanga, mvumbuzi kijana mtanzania ambaye ametengeneza kifaa chenye uwezo wa kusambaza elimu katika mazingira ambayo hakuna mwalimu, akilenga zaidi wanafunzi katika kipindi hiki ambapo shule zimefungwa kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa COVID 19.
Uvumbuzi wa kifaa kwa ajili ya kukabiliana na nyakati za COVID-19
Na sasa tumwangazie Ombeni Sanga, mvumbuzi kijana mtanzania ambaye ametengeneza kifaa chenye uwezo wa kusambaza elimu katika mazingira ambayo hakuna mwalimu, akilenga zaidi wanafunzi katika kipindi hiki ambapo shule zimefungwa kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa COVID 19.
Ombeni kwa miaka kadhaa amekuwa akijihusisha na ufundi wa vifaa mbalimbali vya kielektroniki kabla ya kupata wazo la kuunda kifaa hiki ambacho anasema kinaweza kuwa na walimu wengi kwa wakati mmoja
Watoto vizuizini kote duniani wako hatarini kuambukizwa COVID-19-UNICEF
Maelfu ya watoto ambao kwa sasa wanazuiliwa kwenye nchi kadhaa kote duniani wako katika hatari kubwa ya kuambukiwa virusi vya Corona au COVID-19.
Mkurugenzi mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF, Henrietta Fore anasema watoto wengi wanazuiliwa katika maeneo yenye misongamano yaliyo na uhaba wa lishe, huduma za afya na huduma za usafi ambazo ni mazingira bora kwa kusambaa kwa magonjwa kama COVID-19 na kwamba mlipuko katika moja ya vituo hivi unaweza kutokea wakati wowote. Jason Nyakundi na taarifa kamili
(Jason Nyakundi anaisoma taarifa kamili)
13 Aprili 2020
FLORA NDUCHA : Hujambo na Karibu kusikiliza Jarida kutoka Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa, kutoka hapa Marekani.
JINGLE (04”)
FLORA:Ni Jumatatu ya 13 Aprili mwaka 2020, mwenyeji wako hii leo ni mimi FLORA NDUCHA
1: Watoto walio vizuizini wako katika hatari ya kuambukizwa COVID-19 na wanastahili kuachiliwa
Maelfu ya watoto ambao kwa sasa wanazuiliwa kwenye nchi kadhaa kote duniani wako katika hatari kubwa ya kuambukiwa virusi vya Corona au COVID-19.
Watoto walio vizuizini wako katika hatari ya kuambukizwa COVID-19 na wanastahili kuachiliwa
Maelfu ya watoto ambao kwa sasa wanazuiliwa kwenye nchi kadhaa kote duniani wako katika hatari kubwa ya kuambukiwa virusi vya Corona au COVID-19.
Twasherehekea vipi zama hizi za COVID-19? Guterres ahoji huku akitoa ombi maalum
Kuelekea maadhimisho ya sikukuu ya Pasaka kwa waumini wa kikristo na mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani kwa waumini wa dini ya kiislamu, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ametoa ombi maalum kwa viongozi wa imani zote za dini kuunganisha jitihada zao kusongesha amani duniani kote na kujikita katika lengo moja la kutokomeza COVID19.
Kenya na mikakati ya kukabiliana na COVID-19 wakati idadi ya wagonjwa ikiongezeka
Katika makala ya wiki hii tunakwenda Nairobi nchini Kenya, mwandishi wetu Jason Nyakundi anamulika harakati za kukabiliana na virusi vya Corona au COVID-19 na changamoto zitokanazo na hatua za kudhibiti kusambaa kwa virusi hivyo