Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Taarifa kuhusu Virusi vya Corona

Virusi vya Corona kama dharura ya afya ya umma:Taarifa za UN News Kiswahili
Mlipuko uliripotiwa mara ya kwanza Wuhan China Desemba 31, 2019

Ukurasa huu unaleta pamoja taarifa kuhusu muongozo kutoka kwa Shirika la afya la Umoja wa Mataifa, WHO na Umoja wa Mataifa kuhusu mlipuko wa sasa wa virusi vya corona au COVID-19, ambavyo viliripotiwa mara ya kwanza Wuhan, China mnamo Desemba 31, 2019. Tafadhali tembelea ukurasa huu kupata taarifa za kila siku. WHO inafanya kazi kwa karibu na wataalam wa kimataifa, serikali na wadau kupanua ujuzi wa kisayansi kuhusu virusi hivi vipya, kutokana na jinsi vinavyosambaa na athari zake  na kutoa ushauri kwa nchi na watu, kuhusu hatua za kuchukua kwa ajili ya kulinda afya na kuzuia kuenea kwa mlipuko.

© Julius Mwelu/ UN-Habitat

Hatua zaidi zachukuliwa kukabiliana na COVID-19 nchini Kenya

Kufuatia raia wa Kenya kulalamikia hatua ya Rais wa nchi hiyo kutangaza zuio la kusafiri katika baadhi ya mikoa kwa mfano kuingia jijini Nairobi, Msemaji wa serikali ya Kenya Cyrus Oguna ameieleza idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa kuwa tangazo hilo la rais Uhuru Kenyatta halina nia ya kumuumiza mtu yeyote bali kuwakinga wananchi wote dhidi ya virusi vya corona, COVID-19. Hadi sasa Kenya imethibitisha kuwa na wagonjwa 172 baada ya watu wengine 14 kugunduliwa kuwa na virusi hatari vya corona kwa muda wa saa 24 zilizopita. Jason Nyakundi ametuandalia makala hii akiwa mjini Nairobi.

Sauti
5'26"
UN News/ John Kibego

COVIDI-19 yazua changamoto za kupata huduma za afya Uganda

Kuendelea kusambaa kwa virusi vya Corona, COVID-19 kumezifanya nchi kukaza uzi zaidi katika hatua za kukabiliana na mlipuko huo ikiwemo vikwazo vya watu kutembea na hatua za kuwataka kusalia majumbani. Vikwazo hivi pamoja na kusaidia kudhibiti mlipuko wa COVID-19 lakini pia vimezua changamoto zingine. Mathalani nchini Uganda ambako kuna marufuku ya watu kutembea wagonjwa wengi wameanza kupata changamoto ya kufikia huduma za afya kutokana na maagizo mapya yanayolenga kudhibiti kuenea kwa virusi hivyo kama alivyobaini mwandishi wetu nchini humo John Kibego katika makala hii

Sauti
3'37"
Mazoezi ni muhimu kwa afya.
UNICEF/Vishwanathan

Mashabiki wa mpira wa miguu duniani kote tuunde timu moja dhidi ya COVID-19-WHO na FIFA

Shirikisho la soka ulimwewnguni FIFA limeungana na Shirika la afya la Umoja wa Mataifa WHO katika kuunga mkono kampeni ya #BeActive yaani #Jishughulishe iliyozinduliwa leo katika Siku ya kimataifa ya Umoja wa Mataifa ya michezo kwa ajili ya maendeleo na amani ili kuhamasisha watu kuwa na afya wakiwa nyumbani wakati huu ambao dunia inaungana katika mapambano dhidi ya virusi vya corona, COVID-19, leo na kila siku.