Kijana mtanzania avumbua kifaa kinachoweza kusambaza elimu mahali pasipo na walimu

13 Aprili 2020

Ombeni Sanga, mvumbuzi kijana mtanzania ambaye ametengeneza kifaa chenye uwezo wa kusambaza elimu katika mazingira ambayo hakuna mwalimu, akilenga zaidi wanafunzi katika kipindi hiki ambapo shule zimefungwa kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa COVID 19.

Ombeni kwa miaka kadhaa amekuwa akijihusisha na ufundi wa vifaa mbalimbali vya kielektroniki kabla ya kupata wazo la kuunda kifaa hiki ambacho anasema kinaweza kuwa na walimu wengi kwa wakati mmoja

Ombeni anasema anaanza kwa kuandaa maandishi kutoka vyanzo mbalimbali kisha anarekodi sauti za walimu wakifundisha mada za msingi za masomo kabla ya kuziingiza sauti hizo katika kifaa chake. Anapata wapi vifaa? Anaeleza?

Kijana huyu mbunifu anasema changamoto aliyonayo kwa sasa ni kuwa ili kuzalisha kwa wingi kifaa hiki kinachotumia betri za kawaida na kisichohitaji intaneti,  atalazimika kwenda kiwandani lakini uwezo huo hana kwa sasa. Na sasa kwa mukhtasar hebu tuone kifaa hiki kinavyofanya kazi

Kwa kina zaidi kuhusu uvumbuzi wa Ombeni Sanga, endelea kufuatilia vipindi vyetu. 

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud

Fuatilia Habari: Habari zilizopita za Mada Hii

Hata sisi wachora vibonzo, COVID-19 imeathiri kazi zetu-Nathan Mpangala

Ripoti ya hivi karibuni ilizotolewa na shirika la kazi duniani ILO ambayo inakubaliana na taarifa za shirika la fedha duniani IMF, inaonesha kuwa kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa COVID-19, sekta ya ajira itaathirika kwa kiasi kikubwa na hivyo kuathiri uchumi wa dunia.

Hospitali ya taifa Tanzania, Muhimbili yatenga sehemu maalum kwa ajili ya kunawa mikono

Tanzania kama ilivyo katika mataifa mengine imeweka mikakati kwa ajili ya kudhibiti kuenea kwa virusi vya corona au COVID-19. Hatua mbali mbali zinachukuliwa na serikali na pia mashirika binafsi yanaunga mkono juhudi za serikali. Afisa wa maswasiliano wa kituo cha habari cha Umoja wa Mataifa jijini Dar es Saalam, UNIC ametembelea hospital ya taifa ya Muhimbili kushuhudia baadhi ya mikakati iliyowekwa kama sehemu ya juhudi za kudhibiti kuenea kwa virusi hivyo