Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

13 Aprili 2020

13 Aprili 2020

Pakua

FLORA NDUCHA : Hujambo na Karibu kusikiliza Jarida kutoka Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa, kutoka hapa Marekani.

JINGLE (04”)

FLORA:Ni Jumatatu ya 13 Aprili mwaka 2020, mwenyeji wako hii leo ni mimi FLORA NDUCHA

 

1: Watoto walio vizuizini wako katika hatari ya kuambukizwa COVID-19 na wanastahili kuachiliwa

Maelfu ya watoto ambao kwa sasa wanazuiliwa kwenye nchi kadhaa kote duniani wako katika hatari kubwa ya kuambukiwa virusi vya Corona au COVID-19.

Mkurugenzi mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF, Henrietta Fore anasema watoto wengi wanazuiliwa katika maeneo yenye misongamano yaliyo na uhaba wa lishe, huduma za afya na huduma za usafi ambazo ni mazingira bora kwa kusambaa kwa magonjwa kama COVID-19 na kwamba mlipuko katika moja ya vituo hivi unaweza kutokea wakati wowote. Jason Nyakundi na taarifa kamili

(Jason Nyakundi anaisoma taarifa kamili)

Watoto wanaozuiliwa pia wako katika hata ya kutelekekezwa na kudhulumiwa katika misingi ya kijinsia ikiwa kwa mfano huduma za wafanyakazi zitaathiriwa na janga la COVID-19.

Kote duniani, watoto wako kwenye vizuizi vya kisheria, wengine wakiwa wanazuiwa katika vituo vya uhamiaji, kwa saababua ya mizozo, au wakiwa wanaishi na wazazi wao vizuizini.

Watoto hawa na wale walio katika hatari ya kuambukizwa virusi kutokana na hali zao za afya, kimwili na kiakili wanastahili kuachiliwa.

Tunatoa wito kwa serilikali na mamlaka zingine za kuzuia kuwaachilia kwa dharura watoto wote ambao wanaweza kurudi salama kwa familia zao au kutafuta suluhu ingine.

UNICEF pia inatoa wito wa kusitishwa usajili mpya wa watoto katika vituo vya kuzuia.

UNICEF na muungano wa kuwalinda watoto, wasomi na mashirika ya Umoja wa Mataifa, wametoa mwelekezo wa hatua kuu mamlaka zinaweza kuchukua kuwalinda watoto wakati  huu wa janga la COVID-19.

UNICEF iko tayari kuzisaidia mamlaka  katika maandalizi ya kuwaachilia watoto ikiwemo kutambua mazingira salama.

Haki za watoto kulindwa pamoja na maslahi yao ni lazima vilindwe hususan wakati wa majanga kama sasa. Njia bora ua kulinga haki hii ni kuwaachilia kwa njia salama, ilisema taarifa hiyo ya UNICEF.

 

 

 ===================================================

 

2: Kijana mtanzania avumbua kifaa kinachoweza kusambaza elimu mahali pasipo na walimu

 

Na sasa tumwangazie Ombeni Sanga, mvumbuzi kijana mtanzania ambaye ametengeneza kifaa chenye uwezo wa kusambaza elimu katika mazingira ambayo hakuna mwalimu, akilenga zaidi wanafunzi katika kipindi hiki ambapo shule zimefungwa kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa COVID 19.

 

Ombeni kwa miaka kadhaa amekuwa akijihusisha na ufundi wa vifaa mbalimbali vya kielektroniki kabla ya kupata wazo la kuunda kifaa hiki ambacho anasema kinaweza kuwa na walimu wengi kwa wakati mmoja

 

OMBENI CLIP 1

 

Ombeni anasema anaanza kwa kuandaa maandishi kutoka vyanzo mbalimbali kisha anarekodi sauti za walimu wakifundisha mada za msingi za masomo kabla ya kuziingiza sauti hizo katika kifaa chake. Anapata wapi vifaa? Anaeleza?

 

OMBENI CLIP 2

 

Kijana huyu mbunifu anasema changamoto aliyonayo kwa sasa ni kuwa ili kuzalisha kwa wingi kifaa hiki kinachotumia betri za kawaida na kisichohitaji intaneti,  atalazimika kwenda kiwandani lakini uwezo huo hana kwa sasa. Na sasa kwa mukhtasar hebu tuone kifaa hiki kinavyofanya kazi

 

OMBENI CLIP 3

 

Kwa kina zaidi kuhusu uvumbuzi wa Ombeni Sanga, endelea kufuatilia vipindi vyetu.  

 ====================================================

STUDIO. MIDWAYSTING

====================================================

FLORA: Punde ni makala na leo tunamulika athari za mabadiliko ya tabianchi wilaya ya Pangani mkoani Tanga nchini Tanzania, baki nami.

====================================================

 

3: Mradi wa Mwangaza Mashinani Kenya waua ndege wawili kwa jiwe moja

 

Nchini Kenya, mradi wa pamoja kati ya shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF na wadau wake wa kupatia nishati ya sola kwa wakazi wenye kipato duni vijijini umekuwa ni sawa na kauli ya wahenga wa jiwe moja kuua ndege wawili badala ya ndege mmoja kama ilivyotarajiwa hapo awali. Grace Kaneiya na ripoti kamili.

 

(Taarifa ya Grace Kaneiya)

 

Nats…

 

Ni katika kaunti ya Baringo nchini Kenya, moja ya maeneo ambako mradi wa Mwangaza Mashinain unatekelezwa kwa lengo la kuongeza muda wa watoto kusoma usiku kwa kutumia taa za sola ambazo kaya zao zimepatiwa na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF pamoja na wadau wake.

 

Susan Momanyi, afisa wa UNICEF Kenya anafunga safari kukagua ufanisi wa mradi nyumbani kwa Regina John, mmoja wa wanufaika ambaye ni mama wa watoto watatu, akiwemo Purity ambaye aliugua homa ya uti wa mgongo.

 

Nats. 

 

Punde wanafika kwa Regina ambaye anazungumzia faida za taa za sola kwa masomo ya wanae.

 

(Sauti ya Regina John)

 

“Hapo awali kabla sijapata hicho kifaa, nilikuwa napitia hali ngumu hasa upande wa watoto kusoma watoto pale ndani. Walikuwa hawawezi kusoma nyakati za usiku kwa sababu nilikuwa natumia lile taa la mkopo ambalo lina moshi mkali. Wakati alikuwa hajapata hicho kifaa alama zake zilikuwa ziko chini sana. Saa hii anasoma vizuri na alama zake zimepanda, alikuwa na D+ sasa anapata na B+.”

 

 

Na kisha akaelezea ni kwa vipi mradi ulimgusa pia Purity ambaye ameshapona na ameanza tena masomo..

 

(Sauti ya Regina John)

 

“Na hizo dawa zilikuwa kila baada ya saa 5 umpatie dawa, kila baada ya saa 5 umpatie dawa, na hivyo ulinisaidia sana kwa sababu nilikuwa namwangilia usiku kucha, siwezi ati kutafuta taa kwa sababu hakuna taa. Hilo taa lilkuwa linawaka usiku mzima nikiangalia huyo mtoto.”

 

 

Susan anasema wao UNICEF wanakusanya ushahidi kuona ni kwa vipi mradi huu wa sola unaweza kufikia kaya zenye kipato cha chini zaidi na hata kuongeza muda wa malipo ya vifaa vya sola.  Na zaidi ya yote..

 

(Sauti ya Susan Momanyi)

 

“Unaona mabadiliko, unaona jinsi ambavyo tunabadilisha maisha, unaona ni jinsi gani tunainua familia, na hii ni furaha ya kipekee.”

 

Wadau wengine kwenye mradi huo ni serikali ya Kenya, ubalozi wa Sweden nchini Kenya na Energy 4 Impact.

 

 

===================================================

STUDIO: Play MUSIC 4 for 5 seconds and hold under

====================================================

FLORA: Na sasa ni makala ambapo Saa Zumo wa Radio washirika Pangani FM kutoka Tanga nchini Tanzania anazungumza na Afisa Mifugo wa kata moja wilayani humo kuhusu athari za mabadiliko ya tabianchi, ambapo afisa huyo anaanza kwa kujitambaulisha. 

=================================================

STUDIO: PLAY MAKALA

====================================================

 

ASSUMPTA: Play MUSIC 4 for 5 seconds and hold under

====================================================

FLORA: Shukrani sana Saa Zumo kwa makala hiyo.

 ====================================================

Na sasa ni mashinani, ambapo Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya wanawake, UN-Women, Phuzmile Mlambo-Ngcuka anataka usaidizi zaidi kwa wanawake wauguzi wanaokabiliana na ugonjwa wa virusi vya Corona, au COVID-19.

 

 ===================================================

Studio: Play Mashinani

====================================================

FLORA:Shukrani sana  Bi. Phumzile Mlambo-Ngcuka kwa ujumbe huo 

==================================================

STUDIO: Play Bridge

 

FLORA: Na hadi hapo natamatisha jarida letu la leo. Tupatane kesho kwa habari na makala kutoka Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa unaweza kupata matangazo na taarifa nyingine na kujifunza Kiswahili kwenye wavuti wetu news.un.org/sw. Msimamizi  wa matangazo ni ASSUMPTA MASSOI na mimi ni FLORA NDUCHA, nasema kwaheri kutoka Marekani.

 

==================================================

TAPE: CLOSING BAND

Audio Credit
Flora Nducha
Audio Duration
12'55"