Skip to main content

Watoto walio vizuizini wako katika hatari ya kuambukizwa COVID-19 na wanastahili kuachiliwa

Wavulana wafungwa wakiwa kizuizini, gerezani, Abomey, Benin.
UNICEF/Giacomo Pirozzi
Wavulana wafungwa wakiwa kizuizini, gerezani, Abomey, Benin.

Watoto walio vizuizini wako katika hatari ya kuambukizwa COVID-19 na wanastahili kuachiliwa

Afya

Maelfu ya watoto ambao kwa sasa wanazuiliwa kwenye nchi kadhaa kote duniani wako katika hatari kubwa ya kuambukiwa virusi vya Corona au COVID-19.

Mkurugenzi mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF, Henrietta Fore anasema watoto wengi wanazuiliwa katika maeneo yenye misongamano yaliyo na uhaba wa lishe, huduma za afya na huduma za usafi ambazo ni mazingira bora kwa kusambaa kwa magonjwa kama COVID-19 na kwamba mlipuko katika moja ya vituo hivi unaweza kutokea wakati wowote. 

Watoto wanaozuiliwa pia wako katika hata ya kutelekekezwa na kudhulumiwa katika misingi ya kijinsia ikiwa kwa mfano huduma za wafanyakazi zitaathiriwa na janga la COVID-19.

Kote duniani, watoto wako kwenye vizuizi vya kisheria, wengine wakiwa wanazuiwa katika vituo vya uhamiaji, kwa saababua ya mizozo, au wakiwa wanaishi na wazazi wao vizuizini.

Watoto hawa na wale walio katika hatari ya kuambukizwa virusi kutokana na hali zao za afya, kimwili na kiakili wanastahili kuachiliwa.

Tunatoa wito kwa serilikali na mamlaka zingine za kuzuia kuwaachilia kwa dharura watoto wote ambao wanaweza kurudi salama kwa familia zao au kutafuta suluhu ingine.

UNICEF pia inatoa wito wa kusitishwa usajili mpya wa watoto katika vituo vya kuzuia.

UNICEF na muungano wa kuwalinda watoto, wasomi na mashirika ya Umoja wa Mataifa, wametoa mwelekezo wa hatua kuu mamlaka zinaweza kuchukua kuwalinda watoto wakati  huu wa janga la COVID-19.

UNICEF iko tayari kuzisaidia mamlaka  katika maandalizi ya kuwaachilia watoto ikiwemo kutambua mazingira salama.

Haki za watoto kulindwa pamoja na maslahi yao ni lazima vilindwe hususan wakati wa majanga kama sasa. Njia bora ua kulinga haki hii ni kuwaachilia kwa njia salama, ilisema taarifa hiyo ya UNICEF.