Skip to main content

Nchi 30 na wadau wa kimataifa wajiunga kupiga jeki C-TAP:WHO

Mkurugenzi mkuu wa WHO Dkt. Tedros Ghebreyesus akizungumza katika moja ya taarifa za WHo kuhudsu janga la COVID-19
UN Photo/Evan Schneider
Mkurugenzi mkuu wa WHO Dkt. Tedros Ghebreyesus akizungumza katika moja ya taarifa za WHo kuhudsu janga la COVID-19

Nchi 30 na wadau wa kimataifa wajiunga kupiga jeki C-TAP:WHO

Afya

Nchi 30 na wadau mbalimbali wa kimataifa na taasisi wamejiunga kusaidia mkakati wa fursa za kiteknlojia dhidi ya janga la virusi vya corona au COVID-19 ujulikanao kama C-TAP, mkakati wenye lengo la kufanya chanjo, vipimo, matibabu na teknolojia zingine za kupambana na COVID-19 kupatikana kwa kila mtu, kwa mujibu wa shirika la afya la Umoja wa Mataifa WHO.

Mkakati huo ulipendekezwa kwa mara ya kwanza mwezi Machi na Rais wa Costa Rica Carlos Alvarado ambaye leo amejiunga na mkurugenzi mkuu wa WHO Dkt. Tedros Adhanom Ghebreyesus katika uzinduzi rasmi wa mkakati huo uliofanyika kwa njia ya video mjini Geneva Uswis.

Akizinfua mkakati huo wa C-TAP Dkt. Tedros amesema “Tunayakaribisha makampuni au serikali ambazo zinatengeneza vifaa tiba ili kuchangia muundo wao katika mkakati huu wa tiba ambao baadaye utatoa vibali kwa watengenezaji. Huu ni wakati ambapo watu wanatakiwa kuweka vipeumbele. Nyenzo za kuzuia, kubaini na kutibu COVID-19 ni masuala muhimu kwa umma ambayo yanahitaji kupatikana kwa wote.”

Mkakati wa C-TAP

Kwa mujibu wa WHO fursa ya mkakati wa C-TAP itakuwa ni ya hiyari na ni kwa msingi wa mshikamano. Utatoa fursa ya sehemu moja ambapo patapatikana ujuzi wa kisayansi, takwimu na hati miliki ambavyo vitatumika sawia na jumuiya ya kimataifa.

Rais wa Costa Rica akuzungumza katika uzinuzi huo amesema “Itakuwa haina maana yyoyote kufikia maendeleo haya makubwa ya teknolojia endapo hatutaweza kuhakiki fursa nafuu ya kupata teknolojia hiyo.”

Kwa upande wake Kamishina Mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Michelle Bachelet akiongeza sauti yake amesema “Endapo halitodhibitiwa haraka janga la COVID-19 litaendelea kusambaratisha maisha, biashara na chumi na kutuathiri sote kwa njia moja au nyingine. Hivyo hebu na tujiunge Pamoja kubadilishana takwimu na taarifa, kusongesha mbele uhamishaji wa teknolojia na kupanua wigo wa upatikanaji wa madawa na teknolojia za afya.”

Naye mchumi Joseph Stiglitz amesema “Endapo tutaacha mifumo ya kawaida ya wachache kuhodhi makampuni ya madawa ambao wanasiukuma mbele na kupandisha bei, itamaanisha kwamba wale masikini wawe katika nchi tajiri, za kipato cha wastan au nchi masikini, watashindwa kupata fursa hadi pale tutakapokuwa na mkakati kama huuC-TAP.”

Lengo la C-TAP ni kusongesha mbele uvumbuzi wa chanjo, madawa na teknolojia zingine kupitia utafiti ulio wazi wa kisayansi, na kuharakisha uzalishaji kwa kusanya uwezo wa ziada wa wazalishaji.

Hii itasaidia kuhakikisha kuwepo kwa fursa sawa za bidhaa ambazo tayari zipo na mpya za afya za kukabili COVID-19.