Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Taarifa kuhusu Virusi vya Corona

Virusi vya Corona kama dharura ya afya ya umma:Taarifa za UN News Kiswahili
Mlipuko uliripotiwa mara ya kwanza Wuhan China Desemba 31, 2019

Ukurasa huu unaleta pamoja taarifa kuhusu muongozo kutoka kwa Shirika la afya la Umoja wa Mataifa, WHO na Umoja wa Mataifa kuhusu mlipuko wa sasa wa virusi vya corona au coronavirus">COVID-19, ambavyo viliripotiwa mara ya kwanza Wuhan, China mnamo Desemba 31, 2019. Tafadhali tembelea ukurasa huu kupata taarifa za kila siku. WHO inafanya kazi kwa karibu na wataalam wa kimataifa, serikali na wadau kupanua ujuzi wa kisayansi kuhusu virusi hivi vipya, kutokana na jinsi vinavyosambaa na athari zake  na kutoa ushauri kwa nchi na watu, kuhusu hatua za kuchukua kwa ajili ya kulinda afya na kuzuia kuenea kwa mlipuko.

Wanawake na watoto waliotawanywa kutokana na mapigano  Jebel Marra,  Darfur Kaskazini, wakijihifadhi katika kituo kipya cha Tawilla
OCHA

Sudan Kusini, Sudan, CAR, Libya na Haiti kunufaika na ufadhili wa OCHA/CERF

Taarifa iliyotolewa hii leo na ofisi ya Umoja wa Mataifa inayoshughulikia misaada ya dharura, OCHA imeeleza kuwa Mratibu Mkuu wa misaada ya dharura ya kibinadamu kwenye Umoja wa Mataifa ambaye pia ni mkuu wa, Mark Lowcock, hii leo ameachia dola za kimarekani milioni 25 kutoka mfumo mkuu wa dharura wa Umoja wa Mataifa, CERF kwenda kwa shirika la Umoja wa Mataifa la uhamiaji, IOM ili kusaidia mashirika yasiyo ya kiserikali yaliyoko mstari wa mbele katika kutoa hudua ya afya ya kuokoa maisha, huduma za maji na za kujisafi katika mapambano dhidi ya COVID-19 katika Jamhuri ya Afrika ya kati, Haiti, Libya, Sudan Kusini na Sudan. 

WHO imeshirikiana na nyota Mr Bean ili kuukumbusha umma kuendelea kuwa macho dhidi ya COVID-19
WHO

Mr. Bean aunga mkono vita ya WHO dhidi ya COVID-19

Shirika la afya la Umoja wa Mataifa WHO limeweka wazi hii leo kuwa kwa kushirikiana na makampuni mawili ya utengenezaji filamu wameungana na kuzindua tangazo kwa umma lililomshirikisha mchekeshaji nyota duniani Mr Bean kwa lengo la kuwaelimisha wanajamii kuhusu kujikinga na virusi vya Corona.

Gereza Kuu la Ngaragba nchini CAR limepokea vifaa vya kujikinga na COVID-19 kutoka MINUSCA na UNDP.
MINUSCA

MINUSCA yabisha hodi magerezani CAR

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kuweka utulivu nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, MINUSCA na shirika la mpango wa maendeleo la Umoja wa Mataifa, UNDP wamepatia gereza kuu la Ngaragba msaada wa vifaa vya kusaidia kuepusha kuenea kwa ugonjwa wa virusi vya Corona au COVID-19 gerezani humo.

Sauti
1'53"
Vijana wakiwa wamevaa barakoa wakati wa kuendesha baiskeli kwenye bustani moja huko Büyükçekmece, Uturuki.
UNDP/Levent Kulu

Usivae barakoa wakati unafanya mazoezi-WHO

Wakati ugonjwa wa virusi vya Corona au COVID-19 ukiendelea kuenea katika maeneo mbalimbali duniani huku kwingine ukiwa unadhibitiwa, shirika la afya la Umoja wa Mataifa, linaendelea kutoa madokezi kadhaa ili kuhakikisha kuwa mbinu za kujikinga dhidi ya ugonjwa huo hazigeuki na kuwa mwiba kwa mhusika.