Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wahisani wa kimataifa wakutana kuchangisha fedha kuinusuru Yemen:UN

Familia ikipokea msaada wa chaakula katika kituo cha kusambaza chakula huko Ras al'Arah huko Lahj Governorate nchini Yamen
WFP/Saleh Bahulis
Familia ikipokea msaada wa chaakula katika kituo cha kusambaza chakula huko Ras al'Arah huko Lahj Governorate nchini Yamen

Wahisani wa kimataifa wakutana kuchangisha fedha kuinusuru Yemen:UN

Msaada wa Kibinadamu

Wahisani wa kimataifa wanakutana leo katika mkutano ulioitishwa na Ufalme wa Saudi ana Umoja wa Mataifa ili kuchangisha fedha kwa ajili hatua za kibinadamu kunusuru Maisha ya mamilioni ya watu nchini Yemen.

Mkutano huo unaofanyika kwa njia ya mtandao umewaleta Pamoja zaidi ya serikali 130 na wahisani wengine, mashirika ya kimataifa ya misaada ya kibinadamu na maafisa wa misaada ili kuweka bayana hali halisi ya kibinadamu  inayozorota kwa kasi ambako mbali ya zahma zingine zinazowakabili janga la virusi vya Corona au COVID-19 ni changamoto mpya inayowasibu.

Dola bilioni 1.35 zimeahidiwa leo kwenye mkutano wa ngazi ya juu wa kimataifa wa kuchangisha fedha kwa ajili ya operesheni za kibinadamu nchini Yemen. Akitangaza kiwango hicho mratibu mkuu wa wasuala ya kibinadamu na misaada ya dharura wa Umoja wa Mataifa Mark Lowcock amewashukuru wahisani wote na kusema kilichosalia sasa ni kulipa ahadi hizo haraka iwezekanavyo ili kunusuru zahma kubwa kwa mamilioni ya watu wa Yemen wanaohitaji msaada.

Miaka zaidi ya mitano ya vita imeiach Yemen njiapanda, uchumi umesambaratika na taasisi zote za nchi hiyo karibu zitaporomoka, amesema leo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres kwenye ufunguzi wa mkutano wa uchangishaji fedha kwa ajili ya Yemen na kutoa wito wa kuonyesha mshikamano na watu ambao ni masikini kabisa na walio hatarini zaidi duniani.

Guterres ameongeza kuwa “Watu 4 kati ya 5 wa Yemen ambao ni saw ana watu milioni 24 wanahitaji msaada wa kuokoa Maisha katika moja ya mgogoro mkubwa wa kibinadamu duniani. Watoto milioni 2 Yemen wana ugua utapiamlo uliokithiri ambao unaweza kuwadumaza katika ukuaji wao na kuwaathiri katika Maisha yao yote.”

Kumaliza vita ndio suluhu pekee

Katibu mkuu amesema hata hivyo tangu kuanza kwa mwaka huu takribani watu 80,000 wamelazimika kukimbia makwao na kufanya jumla ya watu waliotawanywa na machafuko kufikia karibu milioni 4, huku ugonjwa wa kipindupindu ukiendelea kutishia Maisha ya watu, ambapo mwaka huu pekee watu 110 wamepata ugonjwa huo na mafuriko ya hivi karibuni yameongeza hatari ya maradhi mengine kama malaria na homa ya kidingapopo.

Mapigano yalishika kasi kote nchini Yemen mwaka 2015 kati ya muungano unaoongozwa na Saudia ukiungwa mkono na serikali inayoungwa mkono na jumuiya ya kimataifa iliyoko Kusini mwa nchi hiyo na kundi lililojihami la Huthi ambalo hujulikana pia kama Ansar Allah likidhibiti mji mkuu Sana’a sanjari na washirika wao.

 Katibu Mkuu amesema hakuna njia nyingine mbadala kwa mgogoro wa Yemen isipokuwa kumaliza vita ili amani irejee na kuwapunguzia madhila mamilioni ya watu wa taifa hilo.

Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa lengo kubwa la mkutano huo wa uchangshaji fedha ni kutangaza ahadi za kifedha kwa ajili ya kuendelea na operesheni za kibinadamu Yemen.

Mkutano huo umekuja wakati ambapo hali kwa raia wengi wa Yemen ni mbaya sana kuliko ilivyowahi kuwa katika wakati wowote ule kwenye historia ya nchi hiyo.

Mipango mingi ya misada ya kibinadamu sasa iko njiapanda kutokana na ukata wa fedha. Hivi sasa Yemen ndio mgogoro mkubwa Zaidi wa kibinadamu duniani ikiwa na watu milioni 24 wanaohitaji msaada na ulinzi na hali inazidi kuwa mbaya kila uchao.

Janga la COVID-19

Mazingira yaliyopo yanaashirikia janga la COVID-19 kusambaa haraka, nchi zima na kuulemea mfumo wa afya. Umoja wa Mataifa na mashirika ya misaada yasiyo ya kiserikali NGOs yanahitaji dola bilioni 2.4 kushughulikia mahitaji ya kibinadamu Yemen hadi mwisho wa mwaka huu ikiwemo dola milioni 180 kwa ajili ya kupambana na COVID-19.

Hali halisi ni kwamba fedha zinapelea kwa kiasi kikubwa na kati ya program 41 za misaada ya kibinadamu Yemen Zaidi ya 30 zitafungwa katika wiki chache zijazo endapo fedha zinazohitajika hazitopatikana na hivyo kuwaacha mamilioni ya watu bila msaada wanaouhitaji ili kuishi.

Mkutano wa leo wa wa ngazi ya juu wa uchangishaji fedha hautaji kiwango maalumkinachotrarajiwa kukusanywa lakini mkutano kama huo mwaka jana ulichangisha dola bilioni 2.6. Lakini Umoja wa Mataifa unasema cha muhimu Zaidi ya ahadi za fedha ni mahitaji ya kulipa kwa haraka ahadi hizo ili kuepesha zahma ya kibinadamu inayonyemelea Yemen.

Hali halisi nchini Yemen

Mashirika ya misaada nchini Yemen yanaendesha operesheni kubwa Zaidi za kibinadamu duniani yakiwafikia zaidi ya watu milioni 10 kila mwezi.

 

Makazi ya muda kwenye eneo la kuhifadhi wakimbizi katika wilaya ya Abs, jimboni Hajjah, nchini Yemen. Eneo hili lipo kilometa 150 kutoka kaskazini mwa jimbo la Hudaydah. (8 Mei 2019)
© UNHCR/Ibrahim Al-Ja’adi
Makazi ya muda kwenye eneo la kuhifadhi wakimbizi katika wilaya ya Abs, jimboni Hajjah, nchini Yemen. Eneo hili lipo kilometa 150 kutoka kaskazini mwa jimbo la Hudaydah. (8 Mei 2019)

 

Na janga la COVID-19 limeongeza uharaka, kiwango na mahitaji yay a kuweza kuendesha operesheni hizo. Na bila fedha Zaidi za ufadhili athari zitakuwa mbaya sana

  • .Hali halisi nchini Yemen ni kwamba ni nus utu ya vituo vya afya  nchini humo ndivyo vinavyofanya kazi. Na vituo hivyo vimezidiwa uwezo na wagonjwa wa COVID-19 na upungufu wa barakoa, glovu na mashine za oksijeni kwa ajili ya kutibu wagonjwa.
  • Wahudumu wengi wa afya walio msitari wa mbele kupambana na ugonjwa huu hawana vifaa vya kujikinga na wengi wao hawapokei mishahara.
  • Kupunguza zaidi msaada wa chakula kutapanua wigo wa baa la njaa hasa wakati huu ambapo mamamilioni ya raia wa Yemen wanategemea msaada wa chakula ili kuishi.
  • Lishe kwa Watoto milioni 1.7 na kina mama wajawazito itapunguzwa na karibu Watoto robo milioni watashuhudia msaada ukipunguzwa au kusitishwa.
  • Timu za kusambaza msaada na vituo vya matibabu kwa Watoto walioathirika na utapiamlo wa kupindukia vitalazimika kupunguza au kufunga kabisa huduma na hivyo kuwaweka mamilioni ya Watoto katika hatari ya kifo.
  • Huduma za maji na usafi matika miji mikubwa ya Yemen zinaweza kusitishwa na kuwaacha mamilioni ya watu katika hatari ya magonjwa yatokanayo na maji kama kipundupindu.
  • Msaada wa kusaka familia na kuziunganisha na Watoto wao, huduma za kisaikolojia na msaada kwa manusura wa ukatili wa kijinsia zitakoma.
  • Wagonjwa wanaohitaji upasuaji au wenye magonjwa sugu kaytika maeneo mengi wataachwa bila huduma wala msaada.
  • Na msaada muhimu kwa maelfu ya watu waliotawanywa, wakimbizi na wahamiaji utapunguzwa au kufutwa kabisa.
     

Ujumbe wa washiriki

Mratibu wa Umoja wa Mataifa wa masuala ya kibinadamu na misaada ya dharura Mark Lowcock amesema “ Hali nchi Yemen ni mbaya sana lakini bado tuna uwezo wa kuwafikia watu. Hata baada ya kuwaondoa wafanyakazi wasio wa lazima tunawafanyakazi wengi waliosalia nchini humo. Kuna maelfu ya wafanyakazi wa misaada raia wa Yemen ambao bado wanafanyakazi na Umoja wa Mataifa, Shirika la msalaba mwekundu na NGOs. Lakini mengi ya mashirika hayo yamesalia na mura mfupi tu kabla ya kuishiwa. Tunawaomba wahisani sio tu kutoa ahadi ya fedha leo lakini kulipa ahadi hizo haraka”.

Mark Lowcock mkuu wa OCHA akihutubia Baraza la Usalama kuhusu hali nchini Yemen.
UN Photo/Manuel Elías
Mark Lowcock mkuu wa OCHA akihutubia Baraza la Usalama kuhusu hali nchini Yemen.

 

Ameongeza kuwa mwaka 2019 wahisani waltoa jumla ya dola bilioni 4 kusaidia operesheni za misaada Yemen. Mwaka 2081 wahisani waliytoa dola bilioni 5.2 tunawashukuru kwa ukaribu wao ukiwemo Ufalme wa Saudia, Marekani , Uingereza , Emarati na wengine.

Kuamkia mkutano huu Umoja wa Mataifa umesema umesaliwa na dola milioni 698 tu kwa ajili ya operesheni zote za misaada Yemen, hivyo dola bilioni 2.4 zinazoombwa na Umoja wa Mataifa ni za kuziba pengo lililosalia hadi mwisho wa mwaka huu.

Naye Dkt. Abdullah Al Rabeeah, mshauri na msimamizi mkuu wa kituo cha msaada wa kibinadamu cha mfalme Salman (KSrelief) amesema “Saudi Arabia imeendelea kuwa mhisani mkubwa wa mipango ya huduma za kibinadamu Yemen na tunaziomba nchi nyingine kujitolea kwa ukarimu zaidi. Tunatiwa wasiwasi mkubwa na ukatili na ukiiukwaji mkubwa dhidi ya ufikishaji misaada ikiwa ni pamoja na kuitorosha, kuiba na kuipeleka kwengineko. KSrelief itaendelea kusaidia majimbo yote Yemen kupitia mashirika ya Umoja wa Mataifa , mashirika ya kimataifa nay a kikanda ya NGOs kwa matumaini kwamba msaada huu utasaidia kupunguza mgogoro wa kibinadamu Yemen.Hebu kwa pamoja tujenge mustakabali bora kwa wale wanaotuhitaji.”