10 Agosti 2020

10 Agosti 2020
Jaridani la Umoja wa Mataifa hii leo na Assumpta Massoi 
- Shirka la Umoja wa mataifa la kuhudumia wakimbizi (UNHCR) nchini Uganda leo limesema limesikitishwa na kifo cha kwanza kabisa cha mkimbizi kutokana na virusi vya corona au COVID-19 tangu mlipuko huo utangazwe nchini humo mnamo Machi mwaka huu.
-Mashirika ya Umoja wa Mataifa yaendelea na juhudi za kuokoa maisha Beirut 
- Watafiti wa malaria barani Afrika wameonya kuwa huenda bara hilo likajikuta katika hali ngumu ya kupambaan na ugonjwa wa malaria unaokatili maisha ya maelfu ya watu kila mwaka na hasa watoto wa chini ya umri wa miaka mitano. 
-Na leo kwenye  makala tutakuwa nchini Uganda kuangazia changamoto ya uvamizi wa wanyama kwa wakazi wa maeneo ya jirani na mbuga na pia njia ya kutumia wadudu nyuki kutatua tatizo hilo.

- Na leo mashinani tutakwenda nchini Somalia kuangazia jinsi Shirika la Umoja wa Mataifa la maendeleo UNDP, livyonasaidia hospitali za Somalia na mradi wa paneli za solar kama njia mbadala ya nishati
 

 
 

 

 
 

 

 

 
Audio Credit:
Assumpta Massoi
Audio Duration:
11'47"

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud