Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

COVID-19 imekuwa na athari mbaya kwa zaidi ya watu wa asili milioni 476 kote ulimwenguni. 

Wizara ya Afya ya Bogotá imetuma muuguzi kwenda katika eneo la Suba, kaskazini mwa Bogotá , Colombia kuwahudumia watu wa jamii za asili.
PAHO/Karen González Abril
Wizara ya Afya ya Bogotá imetuma muuguzi kwenda katika eneo la Suba, kaskazini mwa Bogotá , Colombia kuwahudumia watu wa jamii za asili.

COVID-19 imekuwa na athari mbaya kwa zaidi ya watu wa asili milioni 476 kote ulimwenguni. 

Masuala ya UM

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres kupitia ujumbe wake kwa njia ya video kuhusu siku ya leo ya watu wa asili ambayo huadhimishwa Agosti 9 ya kila mwaka, amesema  ni muhimu kwa nchi kuandaa rasilimali ili kushughulikia mahitaji ya watu wa asili, kuheshimu michango yao na kuheshimu haki zao kujibu mahitaji yao, kuheshimu michango yao na kuheshimu haki zao zisizopingika. 

Bwana Guterres amesema kihistoria, watu wa asili wamepunguzwa na magonjwa yaliyoletwa katika maeneo yao kutoka kwingine, magonjwa ambayo watu hawa hawakuwa na kinga nayo.  

Aidha Katibu Mkuu Guterres ameshauri kuwa ni muhimu kwa nchi kuandaa rasilimali ili kushughulikia mahitaji ya watu wa asili, kuheshimu michango yao na kuheshimu haki zao kujibu mahitaji yao, kuheshimu michango yao na kuheshimu haki zao zisizopingika.  

Guterres amesema, “kabla ya janga la sasa, watu wa asili tayari walikuwa wanakabiliwa na ukosefu wa usawa, unyanyapaa na ubaguzi.  Uhaba wa huduma za kutosha za afya, maji safi na kujisafi, vinaongeza hali ya hatari kwao.  huongeza hatari zao. Watu wa asili hufanya kazi katika shughuli za jadi na uchumi wa kujikimu au katika sekta zisizo rasmi. Haya yote yameathiriwa vibaya na ugonjwa huu.” 

Vile vile Guterres akiangazia upande wa wanawake na watoto amesema wanawake wa asili, ambao mara nyingi ndio watoa huduma wakuu wa chakula na lishe kwa familia zao, wameathiriwa vibaya kwa kufungwa masoko ya kazi za mikono, mazao na bidhaa nyingine na kwamba dunia inapaswa pia kwa haraka ishughulikie shida ya watoto wa jamii za asili ambao hawana fursa ya kuelimika.  

COVID-19 imeathiri mazingira ya watu wa asili  

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa pia kupitia ujumbe wake huo amesema ulimwenguni kote, watu wa asili wamekuwa mstari wa mbele katika kudai hatua za kulinda mazingira na tabianchi. Kukosekana kwa utekelezaji wa ulinzi wa mazingira wakati wa janga la COVID-19, kumesababisha wachimbaji haramu wa madini na wakata magogo, kuingilia  maeneo ya watu wa asili.  

“Watu wengi wa asili wamekuwa waathiriwa wa vitisho na vurugu, na wengi wamepoteza maisha. Pamoja na kukabiliwa na vitisho hivyo, watu wa asili wameonesha uvumilivu wa hali ya juu.” Amesema Bwana Guterres.   

Kikundi cha wanawake wa Mayan Poqoman nchini Guatemala
Antonia Benito
Kikundi cha wanawake wa Mayan Poqoman nchini Guatemala

 

Jamii za asili zimeonesha uimara wakati wa janga la virusi vya corona 

Guterres akieleza namna jamii za asili zilivyoonesha uimara pamoja na kuathiriwa na COVID-19 amesema jamii asilia zilizo na uhuru wa kusimamia ardhi zao, himaya na rasilimali zao, zimehakikisha uhakika wa chakula na utunzaji kupitia mazao na dawa za jadi.  

Akitoa mifano ya baadhi ya jamii hizo, Guterres amesema, “watu wa Karen nchini Thailand wamefufua ibada yao ya zamani ya "Kroh Yee" au kufungwa kwa kijiji ili kupambana na janga hili. Mikakati kama hiyo ya kufunga maeneo, imetumika pia katika nchi nyingine za Asia na Amerika ya Kusini.” 

Mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa ameeleza kuwa kuna kila haja ya kutambua haki za watu wa asili ambako kunamaanisha kuhakikisha ujumuishwaji wao na ushiriki katika kushughulikia COVID-19 na mikakati ya kurejea katika hali nzuri, “tangu mwanzo wa janga hili la ulimwengu, mashirika ya Umoja wa Mataifa yamekuwa yakifanya kazi kutetea haki za watu wa asili. Tumekuwa tukisaidia kulinda afya na usalama na kuhakikisha upatikanaji wa ulinzi wa kijamii na fursa za kiuchumi. Mfumo wa Umoja wa Mataifa bado umeazimia kutekeleza Azimio la Umoja wa Mataifa kuhusu Haki za watu wa asili asilia na kuongeza msimamo wao wa mnepo.” 

Neno la msisitizo kutoka UN Women 

Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na wanawake UN Women Pumzile Mlambo Ngucka amesema wakati serikali ulimwenguni kote zinatengeneza na kutekeleza hatua za kupona na kurejea katika hali nzuri, jamii inahitaji kukumbuka kuwa, kwa sababu ya mazingira ya kihistoria yanayohusiana na sera za kikoloni na za ukoloni mambo leo, wanawake wa jamii za asili wako katika nafasi ndogo ya kuhakikishiwa huduma za afya mathalani kupewa bima za afya. Kwa hivyo wako katika uwezekano mkubwa wa kuathiriwa na hali zilizopo ambazo zinaweza kuzidishwa na virusi. Tathimini ya uchunguzi uliopo kutoka katika nchi 16 za kipato cha chini na cha kati unaonesha kuwa wanawake wa jamii za asili na wasichana barubaru wako katika nafasi ndogo ya kufaidika na huduma za afya na hivyo kuwa na matokeo mabaya ya afya ya uzazi. Katika baadhi ya mazingira, wanawake wa jamii za asili wako katika uwezekano mara mbili ya kufariki dunia kutokana na ujauzito na kujifungua ikilinganishwa na wanawake wa jamii nyingine. 

“Hatua za kuzuia COVID-19 pia zimeunda mazingira ambayo yanayoweza kuzidisha hali mbaya ya wanawake wa asili kuingia katika uhusiano wa kinyanyasaji. Maagizo ya kukaa nyumbani yamefunua janga la kivuli cha unyanyasaji wa majumbani, na wanawake wa asili wana uwezekano mkubwa wa kuathiriwa kuliko wanawake wasio wa asili. Hatua za kudhibiti kusafiri kutoka sehemu moja hadi nyingine zimeminya uwezo wa wanawake kutoa taarifa ya manyanyaso na hatimaye kupata kupata msaada wa kisheria.” Amesisitiza Pumzile Mlambo Ngucka.