Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WHO kutuma wataalamu wake ili kupambana na COVID-19, Afrika Kusini.

Muhudumu wa afya mjini Brazzaville nchini Jamhuri ya Congo akivaa vifaa vya kujinginga dhidi ya Corona
WHO
Muhudumu wa afya mjini Brazzaville nchini Jamhuri ya Congo akivaa vifaa vya kujinginga dhidi ya Corona

WHO kutuma wataalamu wake ili kupambana na COVID-19, Afrika Kusini.

Afya

Shirika la afya la Umoja wa Mataifa WHO, kupitia taarifa yake iliyotolewa hii leo mjini Brazzaville, Congo, Geneva Uswisi na Johannesburg Afrika Kusini, limesema linatuma wataalamu wake 43 wenye utaalamu mbalimbali nchini Afrika Kusini ili kusaidia kupambana na ugonjwa wa COVID-19.  

Kundi la kwanza la wataalamu 17 wanatarajiwa kuwasili hii leo na linajumuisha wabobevu katika udhibiti wa kusambaa kwa magonjwa, wachunguzi, wataalamu wa maambukizi, manunuzi na kadhalika. Mmoja wao ni Dkt David Heymann mtaalamu wa magonjwa ya maambukizi na mtaalamu pia wa afya ya umma na ambaye pia aliongoza kikosi cha kupambana na homa ya mafua ya SARS mnamo mwaka 2003.  

Matumizi haya yametokana na majadiliano yanayoendelea kati ya Waziri wa Afya, Mhe Dkt Zweli Mkhize, na uongozi wa WHO na wa kimataifa. Pamoja na Afrika Kusini sasa kuwa kati ya nchi tano za juu zilizoathiriwa zaidi ulimwenguni, ni muhimu kuimarisha majibu yake ya COVID-19. 

Hatua hii imefikiwa kutokana na majadiliano yanayoendelea kati ya Waziri wa Afya, Dkt Zweli Mkhize na uongozi wa kimataifa na kikanda wa WHO. Afrika Kusini ikiwa ni moja ya nchi tano zilizoathirika zaidi na COVID-19, ni muhimu kuimarisha mapambano yake dhidi ya COVID-19. 

Dkt Owen Kaluwa ambaye anaiwakilisha WHO nchini Afrika Kusini anasema, “kwa wakati huu ambao janga la COVID-19 nchini Afrika Kusini linasambaa kwa haraka, ni muhimu kwamba tufanye kazi pamoja ili kuimarisha mapambano yetu dhidi ya virusi. Kwasababu hii, WHO  inaandaa msaada kuongeza nguvu katika juhudi za serikali  za kupambana na COVID-19. Hii ni njia ambayo tutapunguza kusambaa na madhara ya COVID-19.”  

Dk Matshidiso Moeti, Mkurugenzi wa Kanda wa WHO Afrika na Dk Michael Ryan kwa kushirikiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Programu ya Dharura ya Afya ya WHO watafanya kazi kwa ukaribu kutokea Brazzaville, Jamhuri ya Congo na Geneva, Uswisi ili kuwasaidia wataalamu watakaokuwa mstari wa mbele nchini Afrika Kusini.