Skip to main content

Licha ya changamoto waalimu, wazazi na wanafunzi wadhamiria kusoma wakati wa COVID-19 Uganda

Licha ya changamoto waalimu, wazazi na wanafunzi wadhamiria kusoma wakati wa COVID-19 Uganda

Pakua

Ugonjwa wa Corona au COVID-19 ukiendelea kusababisha baadhi ya nchi kufunga shule na vyuo na hivyo wanafunzi kulazimika kusomea majumbani, walimu, wazazi na wanafunzi nchini Uganda, wamezungumzia changamoto wanazokumbana nazo kama anavyoelezea Ahimidiwe Olotu. 

Kutana na Mwalimu Irene wa shule ya msingi ya Clarke iliyoko jijini Kampala nchini Uganda. Anasema kuwa serikali ilipoamua kufunga shule, hilo lilikuwa jambo la kushangaza na ilkuwa ni mazingira tofauti kabisa kwa wazazi na wanafunzi,“watoto wetu hawakuwa wamezoea kuchapa maneno. Wazazi wengi hawakuwa na kompyuta mpakato. Badala yake walikuwa na simu za rununu, na ndipo tukaonea tutumie apu ya WhatsApp” 

Hata hivyo bado kuna changamoto,  Edrien mwanafunzi katika shule ya Clarke mwenye umri wa miaka 11 anasema kuwa changamoto kubwa ni kwamba hana simu ya rununu. 

Kwa kuwa familia yao haina simu ya rununu, baba mzazi wa Edrien ambaye ni dereva wa bodaboda na sasa hafanyi kazi kutokana na COVID-19, analazimika kwenda shuleni kuchukua kazi za shule za mwanae, “robert ni miongoni mwa wazazi, na anaishi mbali na shule kwa hiyo ni lazima asafiri umbali mrefu. Kwa hiyo anasaidia wanae nyumbani kwa kuwa wanashindana na wanafunzi wengine” 

Kwa Edrien awali alikuwa na hofu kuwa kitendo cha baba yake kwenda kufuata nyaraka shuleni, angaliwaletea virusi vya corona, lakini haikuwa hivyo na zaidi ya yote anasema kuwa anafurahi kwa kuwa baba yake anamsaidia sana.

Sasa masomo yanaendelea na baba anamuuliza Edrien atafute neno jipya kwenye kamusi na analiona na kisha Robert ambaye ni baba mzazi anasema, "unafahamu katika huu ulimwengu, kama hujaelimika, maisha ni magumu mno.  Kwa hiyo lazima ujitahidi sana ili watoto wako waende shule kwa maisha mazuri ya baadaye. Shule ni mbali, natumia kati ya dakika 45 hadi 50 kufika shule. Lakini shule ile ina elimu bora. ”

 

Audio Credit
UN News/UNIC DAR-Ahimidiwe Olottu
Sauti
1'49"
Photo Credit
UNICEF/Habib Kanobana