Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ajabu mswahili kupuuza lugha yake- Prof. Mutembei

Kambi za Sayansi katika STEM (Kenya) za kushauri Wasichana kwamba wanaweza masomo ya sayansi. Picha: © UNESCO/ Alice Ochanda

Ajabu mswahili kupuuza lugha yake- Prof. Mutembei

Utamaduni na Elimu

Lugha yako ndio mkombozi wako!  Ikiwa leo ni siku ya Afrika, lugha za asili za Afrika nazo zimepigiwa chepuo na miongoni mwao ni lugha ya Kiswahili ambayo barani Afrika pekee inaongoza kwa kuzungumzwa na watu wengi zaidi, idadi ikitajwa kuwa ni zaidi ya watu milioni 200.

Akizungumzia nafasi ya lugha hiyo katika kuchagiza maendeleo barani humo, Profesa Aldin Mutembei wa Taasisi ya Taaluma za lugha ya Kiswahili ya Chuo Kikuu cha Dar es salaam, TATAKI amesema hilo linawezekana iwapo vijana watapatiwa fursa ya kusoma masomo ya sayansi na teknolojia kwa lugha yao hiyo ya asili.

Profesa Mutembei akasema ingawa baadhi ya waswahili wanapuuza lugha hiyo, mataifa mengine Afrika kwa kutambua umuhimu wake wanaienzi na punde yatakuwa na wabobezi akisema..

Hivi karibuni ilielezwa kuwa lugha ya Kiswahili inaongoza kwa kuwa lugha ya asili inayozungumzwa na watu wengi barani Afrika ikifuatiwa na kihausa halafu kiyoruba.