Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

COP26

COP26: 31 Oktoba-12 Novemba 2021 | Glasgow, Uingereza

Kwa takribani miongo mitatu, Umoja wa Mataifa (UN) umekuwa ukileta pamoja kila nchi duniani kwenye mikutano ya ngazi ya juu kuhusu tabianchi, mikutano ikipatiwa jina COP yaani conference of Parties kwa kiswahli wanachama wa mkutano. Tangu wakati huo, mabadiliko ya tabianchi yamebadilika kutoka suala la  pembezoni hadi kipaumbele cha kimataifa.
 
Mwaka huu utakuwa mkutano wa 26 wa nchi wanachama wa mikutano hiyo, ikipatiwa jina COP26. Uingereza ndio Rais wa mkutano hou wa COP26 na unafanyika Glasgow, Scotland.
Kuelekea COP26, Uingereza inafanya kazi na kila taifa kufikia makubaliano ya jinsi ya kukabili mabadiliko ya tabianchi. Viongozi wa dunia wanawasili Scotland, sambamba na makumi ya maelfu ya washauri, wawakilishi wa serikali, sekta ya biashara, wananchi kwa ajili ya mkutano huo wa siku 12.
Si tu kwamba ni jukumu kubwa, bali pia ni tofaauti na mikutano mingine iliyotangulia ya nchi wanachama wa mkataba wa mabadiliko ya tabianchi. Wataalamu wengi wanaamini kuwa COP26 ni dharura ya kipekee.
Ili kupokea taarifa za kila wakati moja moja kwenye akaunti yako ya barua pepe, tafadhali hakikisha  unajisajili hapa kwenye mada kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres akizungumza na vyombo vya habari kwa njia ya video kuhusu mategemeo yake kwa mkutano wa G7 unaofanyika nchini Uingereza.
United Nations

Chanjo zinapaswa kuzingatiwa kama "bidhaa za umma ulimwenguni" - Guterres 

Akiongea kupitia video huko London, Uingereza, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres amesema hakuna njia nyingine ya kushinda virusi vinavyoenea katika nchi zinazoendelea "kama moto wa nyikani" na hatari za kubadilika, isipokuwa kwa njia ya usawa, chanjo kwa watu wengi, na kuongeza kuwa chanjo zinahitajika "kupatikana na za bei nafuu kwa wote ”