Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chanjo zinapaswa kuzingatiwa kama "bidhaa za umma ulimwenguni" - Guterres 

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres akizungumza na vyombo vya habari kwa njia ya video kuhusu mategemeo yake kwa mkutano wa G7 unaofanyika nchini Uingereza.
United Nations
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres akizungumza na vyombo vya habari kwa njia ya video kuhusu mategemeo yake kwa mkutano wa G7 unaofanyika nchini Uingereza.

Chanjo zinapaswa kuzingatiwa kama "bidhaa za umma ulimwenguni" - Guterres 

Afya

Akiongea kupitia video huko London, Uingereza, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres amesema hakuna njia nyingine ya kushinda virusi vinavyoenea katika nchi zinazoendelea "kama moto wa nyikani" na hatari za kubadilika, isipokuwa kwa njia ya usawa, chanjo kwa watu wengi, na kuongeza kuwa chanjo zinahitajika "kupatikana na za bei nafuu kwa wote ” 

"Ni kwa masilahi ya kila mtu kwamba kila mtu apate chanjo, mapema kuliko baadaye," Katibu Mkuu Guterres amesema, "kwa bahati mbaya, hadi sasa, imekuwa hakuna usawa na si kwa haki  sana jinsi chanjo inavyofanyika ulimwenguni, lakini ninafarijika na matangazo ambayo yametolewa wakati wa mkutano huu wa G7." 

Matangazo hayo ni pamoja na pendekezo la IMF la dola bilioni 50 za kimarekani kumaliza janga la COVID-19 mnamo mwaka 2022 pamoja na ahadi ya uchangiaji wa chanjo milioni 500. 

"Tunapaswa kutambua kuwa tuko vitani na virusi, virusi ambavyo ni hatari sana ambavyo vinasababisha mateso makubwa na kuharibu mitazamo mingi ya maendeleo katika uchumi wa ulimwengu," Guterres amesema. "Na kushinda virusi na kuweza kukuza silaha zetu dhidi ya virusi na muhimu zaidi ya silaha hizo ni chanjo. Na kukuza silaha hizo tunahitaji kuchukua hatua na mantiki, kwa maana ya uharaka na kwa vipaumbele vya uchumi wa vita. Na bado tuko mbali kufika huko.” 

Mbali na COVID-19, jambo lingine muhimu kwenye ajenda ya Mkutano wa G7 ni mabadiliko ya tabianchi. Katibu Mkuu amesema kuwa ongezeko la wastani wa joto kwa kulinganisha na viwango vya awali vya kabla ya maendeleo ya viwanda tayari ni digrii 1.2, karibu sana na digrii 1.5 ambazo wanasayansi wanakubali ni kizingiti ambacho kinaweza kushinikiza ulimwengu katika janga lisiloweza kurekebishwa. 

"Kwa kiwango fulani tuko karibu na shimo, tunahitaji kuhakikisha kuwa hatua inayofuata iko kwenye mwelekeo sahihi," Guterres amesema. 

Ameongeza akisema, "ukweli ni kwamba nchi zilizoendelea bado hazijatimiza ahadi ambazo zilitolewa Paris na ambayo ni kuhusiana na uhamasishaji wa msaada wa dola bilioni 100 za Kimarekani kila mwaka kwa nchi zinazoendelea. Na kwa hivyo, moja ya mambo ambayo ninaamini ni muhimu sana kwa mtazamo wa G7 na nchi za G7, ni kufafanua jinsi bilioni hizi 100 zitatekelezeka. Mnamo 2020, haikutokea. Lazima ifanyike mnamo 2021 na kuendelea, na hii ni jambo muhimu sana kuhakikisha kuwa tuna COP 26 iliyofanikiwa.” 

Katibu Mkuu Guterres amehitimisha ujumbe wake kwa G7 akisema, "Muungano wa Net Zero, umoja wa kimataifa wa 2050 kushughulikia mahitaji ya ulimwengu unaoendelea kuhusiana na fedha kulingana na ahadi zilizotolewa katika Mkataba wa Paris, na mkazo mkubwa kuhusu utekelezajiu ni vipaumbele vitatu ambavyo ningependa kuona nchi za G7 zinajitolea kikamilifu.”