Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Makala

UN/maktaba

Majuto mjukuu, kijana tambua ujana ni maji ya moto

Nchini Thailand kile kilichoonekana kuwa ni raha ya aina  yake kwa msichana mmoja baada ya kukutana na mpenzi wake kupitia mtandao wa kijamii, kimegeuka shubiri baada ya kujikuta na ujauzito bila kujua cha kufanya. Mtoto huyo wa kike aitwaye jina la Fang alikata tamaa ya maisha na kujilaumu kila uchao. Hata hivyo kupitia mradi wa makazi ya dharura unaoungwa mkono na shirika l aUmoja wa Mataifa la idadi ya watu, UNFPA mtoto Fang sasa ameweza kuona nuru kwenye maisha  yake. Je nini kimefanyika? Ungana basi na Assumpta Massoi kwenye makala hii.

Sauti
4'6"
Picha ya IFAD/Santiago Albert Pons

Wachuuza nyanya na mboga mboga ili kujinasua kutoka lindi la umaskini

Umoja wa Mataifa  na wadau wake unachagiza maendeleo ili kubadili maisha ya wakazi wa dunia hii ikiwemo kutokomeza umaskini. Na ndio maana chombo hicho kilipitisha malengo ya maendeleo endelevu,. SDGs ambapo lengo namba moja ni la kutokomeza umaskin ifikapo mwaka 2030. Ni kwa kuzingatia hilo wanawake wa wilaya ya Lwengo, Kusini mwa Uganda nao wameamua kujifunga kibwebwe kuweza kutokomeza umaskini.  Wameanzisha soko lao ambalo linauza bidhaa mbalimbali za matunda kama vile nyanya , na mboga za majani. Siraj Kalyango alivinjari eneo hilo na kukuandalia makala ifuatayo.

Sauti
3'32"
Picha: UNHCR/Video capture

Michezo yawa daraja la kuwanganisha vijana Somalia

Michezo na sanaa imekuwa daraja muhimu la kuwaunganisha wasomali hususan vijana ambao vita vya miaka nenda miaka rundi viliwakatisha tamaa ya mustakhbali wao. Mpango wa Umoja wa Mataifa nchini humo UNSOM kwa kutambua umuhimu wa michezo sio tu kwa kuwaleta watu pamoja bali katika mchakato wa kusaka amani , ukishirikiana na wizara ya michezo ya Somalia uliandaa mashindano ya riadha kwa vijana Somalia siku ya kimataifa ya michezo kwa ajili ya amani na maendeleo.

Sauti
3'48"

Bima ya afya ni muarobaini wa afya kwa wote- Dkt. Maro

Upatikanaji wa bima ya afya kwa kila mtu ni suala mtambuka  ambalo Umoja wa Mataifa na mashirika yake , wameendelea kulipigua chepuo ili ifikapo mwaka 2030 kila mtu bila kujali rika, uwezo au rangi yake ana uwezo wa  kununua bima ya afya. Utekelezaji wa hoja hiyo unaenda sambamba na mpango wa kimataifa wa kuhakikisha kila mtu anapata huduma ya afya popote pale alipo, UHC au Universal Health Coverage.

Sauti
4'1"

Kazi ni kazi ilimradi inafanywa kwa ustadi

Katika ajenda ya maendeleo endelevu ya mwaka 2030 , lengo namba 5 la usawa kijinsia, suala ambalo linahimiza jamii kote duniani kuwajumuisha wanawake katika kazi yoyote bila kubagua jinsia, rangi, au rika ya mtu.

Mwandishi wetu anatuletea mfano mzuri nchini kenya  ambako wasichana wameanza kujikita katika kazi ambazo zimezoweleka kufanywa na wanaume. Msichana Tsarah Mumbi kwa sasa ni kivutio kikubwa kwa kila mtu kwa chaguo la kazi analofanya. Unagana na mwandishi wetu kwa undani wa makala hii.

 

Sauti
3'44"
UN News/Assumpta Massoi

Ukombozi wa mwanamke kijijini utategemea ushirikiswahi wake:FAO

Ili kuweza kumkomboa mwanamke wa kijijini, ni lazima ashirikishwe katika mchakato mzima, kuanzia utungaji wa sera hadi umilikaji wa ardhi.

Wito huo umetolewa na Bi Susan Kaaria afisa wa masuala ya jinsia katika idara ya sera ya shirika la chakula na kilimo FAO.

Katika makala hii anajadili na Flora Nducha, kama FAO wanafanya nini kufanikisha azma hiyo Ungana nao.

Sauti
3'9"
UN Photo/Sophia Paris

Taka zaepusha matumizi ya dizeli Uganda

Matumizi ya nishati mbadala na salama ni jambo ambalo linapigiwa chepuo na Umoja wa Mataifa ambapo lengo namba 7 la malengo ya maendeleo endelevu, SDGs linasisitiza nishati rahisi na salama. Hatua hii inazingatia kwamba idadi ya watu wanaohitaji nishati ya umeme inaongezeka kila siku na hivyo kutoa changamoto ya kusaka vyanzo mbadala vya nishati kwani umeme pekee uliozoeleka ni wa vyanzo vya maji, na ukame unatishia uwepo wa mabwawa ya maji. Ni kwa kuzingatia hilo huko Uganda, wanatumia mabaki ya taka au biomasi ili kuzalisha nishati. Je nini kinafanyika?

Sauti
3'16"
Picha: Luca Renda / UNDP

Utu wetu hudhiirika tunapowasaidia wenye shida

Majanga yanapotokea hua hayapigi hodi, na tunapoamua kuwasaidia waathirka ni jambo jema kwani huo ndio utu wetu. Umoja wa Mataifa na mashirika wadau wamekuwa mstari wa mbele katika kutoa usaidizi wakati wa migogoro ya kivita, majanga na matatizo  mbambali yanapotokea duniani kote.

leo katika ukumbi wa mikutano wa Umoja wa Mataifa, wafadhili , wahisani  na wageni waalikwa wamekusanyika kutoa usaidizi kwa wahanga wa kimbunga Maria katika visiwa vya karibea mwaka jana . 

Sauti
4'14"