Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Makala

UNOCHA/Emmi Antinoja

Kuangazia suluhisho kutabadilisha hali katika eneo hili tete la Sudan na Sudan Kusini -Filippo Grandi

Kupata suluhisho zinazotegemea amani na maendeleo ni muhimu kwa mustakabali wa watu karibu milioni saba waliolazimika kuhama kwa lazima makwao kutoka Sudan na Sudan Kusini, amesema kamishna mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR Filippo Grandi kufuatia ziara yake ya siku tatu katika mwezi huu wa Agosti kwenye nchi hizo mbili, ziara ambayo imeweka wazi kuwa watu wanaorejea kutoka ukimbizini katika nchi hizo wanarudi na kukuta nyumba zao zimeharibiwa, na miundombinu haitoshi au hakuna huduma za kijamii.

Sauti
3'22"
UNICEF/UN014189/Sang Mooh

Tunaamini tukimsaidia kijana mmoja, atarudi kuwasaidia wengine-Pendo Afrika

Maisha ya vijana huchukua mikondo tofauti pindi wanapokosa usimamizi ulio bora na hivyo kujikuta katika changamoto kama vile madawa ya kulevya. Pia mila na tamaduni mbalimbali zinarudisha nyuma hatua ambazo zimeshapigwa katika kuleta usawa wa kijinsia na kuwaweka watoto wa kike katika mazingira ya mimba za utotoni. Lakini pamoja na hayo, watu mmoja mmoja na hata kwa makundi, taifa na hata kwa ushirikiano wa kimataifa, bado wana ari ya kutimiza malengo ya Umoja wa Mataifa ya maendeleo endelevu, SDGs kwa kuhakikisha hakuna anayeachwa nyuma.

Sauti
3'58"
UNICEF/Catherine Ntabadde

Nimepumzisha kazi yangu ya uuguzi ili nipiganie haki za wasichana Pokot, Kenya - Everline Prech

Katika baadhi ya jamii barani Afrika bado zipo tamaduni  ambazo kwa kiasi kikubwa zinawakandamiza wasichana na pia wanawake ingawa ipo mikakati mingi ya kupambana na tamaduni hizo na matunda yanaanza kuonekana. Mwandishi wetu wa Kenya, Jason Nyakundi amemhoji  Everline Prech, mwanaharakati anayepiga vita tamaduni  potovu zinazowakandamiza wasichana na wanawake katika jamii ya Pokot nchini Kenya, jambo ambalo likifanikiwa litakuwa limetoa mchango katika kufikia malengo ya Umoja wa Mataifa ya maendeleo endelevu, SDGs kufikia kilele chake mwaka 2030.

 

Sauti
3'27"
UN Photo/Logan Abassi

Kijana msomi ageukia ufugaji wa nzi ili kunusuru wafugaji wa samaki 

Vijana katika sehemu mbalimbali duniani wameitikia wito wa Umoja wa Mataifa wa kubonga bongo na kusongesha maendeleo yao pale walipo kwa kubaini suluhisho la changamoto zinazokabili jamii inayowazunguka. Miongoni mwao ni Dayana Olembe kutoka Tanzania ambaye baada ya kubaini kuwa wafugaji wa kuku na samaki wanapata shida kupata protini ya kile wanachofuga, akaamua kuingia katika biashara ya ufugaji wa nzi. Ni kweli utashangaa nzi? Ndio!

Sauti
4'36"
UN Women/Ploy Phutpheng

Ufadhili wa Benki ya Dunia, wawasaidia kiuchumi wananchi wa Thailand dhidi ya athari za Covid-19

Kutokana na kuyumba kwa uchumi nchini Thailand kulikosababishwa na mlipuko wa ugonjwa wa Covid-19 na kuathiri ajira, kipato na hivyo kuongeza umaskini, hatua za haraka za serikali kwa kushirikiana na Benki ya Dunia zimesaidia wananchi kutoangukia katika ufukara. Hali ilikuwa mbaya kiasi kufikia robo ya kwanza ya mwaka 2021 kulikuwa na upungufu wa kazi 710,000 kuliko ilivyokuwa katika robo ya nne ya mwaka 2020. Kiasi cha ufadhili kilichotolewa, asilimia 70 ilipelekwa katika kaya zenye uhitaji zaidi na kiasi kidogo kilichosalia kikaelekezwa katika sekta binafsi.

Sauti
3'10"
UNDP/Sawiche Wamunza

Changamkieni kilimo cha maharage machanga kuinua kipato na kuondoa umaskini- Hadija

Vijana wameitikia wito wa  Umoja wa Mataifa wa kuchukua dhima ongozi katika kufanyia marekebisho na hatimaye kuboresha mifumo ya uzalishaji wa vyakula. Hii ni kuanzia shambani hadi mezani ili hatimaye ifikapo mwaka 2030 suala la ukosefu wa chakula au njaa lisalie kuwa historia sambamba na mifuko ya watu iwe imetunishwa kupitia kilimo bora na cha kisasa, na hivyo kufanikisha lengo la kwanza la malengo ya maendeleo endelevu ya Umoja wa Mataifa, SDGs, la kutokomeza umaskini.

Sauti
4'24"