Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ufadhili wa Benki ya Dunia, wawasaidia kiuchumi wananchi wa Thailand dhidi ya athari za Covid-19

Ufadhili wa Benki ya Dunia, wawasaidia kiuchumi wananchi wa Thailand dhidi ya athari za Covid-19

Pakua

Kutokana na kuyumba kwa uchumi nchini Thailand kulikosababishwa na mlipuko wa ugonjwa wa Covid-19 na kuathiri ajira, kipato na hivyo kuongeza umaskini, hatua za haraka za serikali kwa kushirikiana na Benki ya Dunia zimesaidia wananchi kutoangukia katika ufukara. Hali ilikuwa mbaya kiasi kufikia robo ya kwanza ya mwaka 2021 kulikuwa na upungufu wa kazi 710,000 kuliko ilivyokuwa katika robo ya nne ya mwaka 2020. Kiasi cha ufadhili kilichotolewa, asilimia 70 ilipelekwa katika kaya zenye uhitaji zaidi na kiasi kidogo kilichosalia kikaelekezwa katika sekta binafsi. Lucy Igogo anaeleza zaidi. 

Audio Credit
Assumpta Massoi/Lucy Igogo
Sauti
3'10"
Photo Credit
UN Women/Ploy Phutpheng