Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Zamani haikuwa rahisi kwa mwanamke kuingia katika utangazaji kama leo - Khadija Ali, KBC

Zamani haikuwa rahisi kwa mwanamke kuingia katika utangazaji kama leo - Khadija Ali, KBC

Pakua

Usawa wa kijinsia ni ajenda ambayo imeendelea kupiganiwa na Umoja wa Mataifa kila uchao. Ingawa ajenda hiyo imekuwa ikikumbwa na vikwazo kulingana na tamaduni za muda mrefu za baadhi ya maeneo duniani, hatua zimepigwa na tayari jamii zinabadilika na kuanza kuukumbatia usawa wea kijinsia kati ya mwanamke na mwanaume. 

Kuangazia hilo tuelekee nchini Kenya ili kuona ilikuwa vigumu kwa njia gani mwanamke kujiunga na fani ya utangazaji miaka ya 1970 ikilinganishwa na sasa? Kwenye makala ya leo mwandishi wetu wa Kenya, Jason Nyakundi amemhoji  Mama Khadija Ali, mtangazaji maarufu wa miaka mingi  nchini Kenya. Mama Khadija alijiunga na shirika la serikali KBC mwaka 1974 wakati huo likijulikana kama VOK, au Sauti ya Kenya na hadi sasa anavuma hewani.  Khadija pia anawapa ushauri wanawake kuhusu namna ya kuweza kufanikiwa katika fani ya utangazaji.

Audio Credit
Assumpta Massoi/Jason Nyakundi
Audio Duration
3'35"
Photo Credit
Picha ya UNAMID/ Hamid Abdulsalam