Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wanawake katika jamii ya Watwa ndio hasa nguzo ya jamii licha ya kukandamizwa – Vital Bambanze

Wanawake katika jamii ya Watwa ndio hasa nguzo ya jamii licha ya kukandamizwa – Vital Bambanze

Karibu msikilizaji wetu wa Habariza UN. Mimi ni Anold Kayanda. Katika mahojiano haya nami, utamsikia Vital Bambanze ambaye ni Mkurugenzi wa shirika la UNIPROBA linalohusika na kutetea haki za watu wa kabila la Watwa nchini Burundi na hivyo kusongesha matamanio ya Umoja wa Mataifa ya kuhakikisha kunakuwa na usawa kote duniani na hakuna anayeachwa nyuma katika maendeleo ya ulimwengu. Bambanze pia ni mjumbe wa jukwaa la kudumu la Umoja wa Mataifa wa watu wa asili, akizungumza nami mjini New York Marekani, anaeleza nafasi ya wanawake kwenye jamii hiyo.
Pakua
Audio Credit
Anold Kayanda
Audio Duration
3'36"
Photo Credit
UN/Assumpta Massoi