Tanzania inajitahidi kujumuisha wanawake katika TEHAMA: Injinia Ichokeleza
Sekta ya habari na mawasiliano kwa muda mrefu hasa kwenye mataifa yanayoendelea imekuwa ikitawaliwa na wanaume. Lakini katika zama hizi za utandawazi na umuhimu wa malengo ya maendeleo endelevu, SDGs yanayohimiza yeyote asiachwe nyuma na treni ya maendeleo ya 2030. Nchi zimeanza kuchukua hatua kwa chagizo la Umoja wa Mataifa kujumuisha wanawake katika TEHAMA. Nchini Tanzania serikali imeweka mikakati ikihusisha kuhamasisha jamii wakiwemo wazazi kuwachigiza watoto wao wa kike kuingia katika masomo yahusianayo na TEHAMA.