Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tanzania inajitahidi kujumuisha wanawake katika TEHAMA: Injinia Ichokeleza

Tanzania inajitahidi kujumuisha wanawake katika TEHAMA: Injinia Ichokeleza

Pakua

Sekta ya habari na mawasiliano kwa muda mrefu hasa kwenye mataifa yanayoendelea imekuwa ikitawaliwa na wanaume. Lakini katika zama hizi za utandawazi na umuhimu wa malengo ya maendeleo endelevu, SDGs yanayohimiza yeyote asiachwe nyuma na treni ya maendeleo ya 2030. Nchi zimeanza kuchukua hatua kwa chagizo la Umoja wa Mataifa kujumuisha wanawake katika TEHAMA. Nchini Tanzania serikali imeweka mikakati ikihusisha kuhamasisha jamii wakiwemo wazazi kuwachigiza watoto wao wa kike kuingia katika masomo yahusianayo na TEHAMA. Injinia Clarence Ichokeleza mkurugenzi wa mawasiliano katika wizara ya ujenzi, uchukuzi na mawasiliano nchini humo amemfafanulia Flora Nducha wa Idhaa hii kuhusu hatua hizo

Audio Credit
Grace Kaneiya/ Flora Nducha/ Clarence Ichokeleza
Audio Duration
4'49"
Photo Credit
ITU