Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

CIAT na utafiti wa maharage nchini Uganda

CIAT na utafiti wa maharage nchini Uganda

Pakua

Katika kurejelea baadhi ya habari zilizokuwa na mvuto zaidi mwaka uliopita wa 2018, tunarejea nchini Uganda hususan kwenye kituo cha kimataifa cha utafiti wa kilimo kwa nchi za kitropoki, CIAT ambako tulizungumza na Robin Buruchara, mtafiti wa maharagwe katika kituo hicho.

Siraj Kalyango wa Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa alizungumza naye kuweza kubaini pamoja na mambo mengine aina za maharagwe na jukumu la utafiti na faida zake. Lengo ni kuona ni kwa jinsi gani kituo hicho kinasaidia katika kuboresha kilimo cha maharage na pia kuona ni jinsi gani wanaweza kuwa na mbegu zinazohimili magonjwa na hivyo kusaidia kufanikisha malengo ya maendeleo endelevu, SDGs namba 1 la kutokomeza umaskini na namba 2 la kuondokana na njaa.

Kwa kina basi ungana nao ambapo Bwana Buruchara anaanza kwa kufafanua kazi ya CIAT.

Audio Credit
Grace Kaneiya/ Siraj Kalyango
Audio Duration
4'10"
Photo Credit
FAO/Claudia Nicolai