Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Nina furaha sasa naweza kuzalisha mazao kwa mwaka mzima- Mkulima

Nina furaha sasa naweza kuzalisha mazao kwa mwaka mzima- Mkulima

Pakua

Kilimo ndio uti wa mgongo wa mataifa mengi yanayoinukia hususan barani Afrika. Lakini mabadiliko ya tabianchi yanawaletea hofu kwani hukwaza maendeleo ya kilimo ambacho ni tegemeo lao kuu. Lakini  pamoja na kuleta hofu kwa wakulima kutokana na ugumu wa kilimo na kutatiza uzalishaji wa mazao mbalimbali, kwa wengine mabadiliko ya tabianchi huwapa changamoto ya kubuni njia mbadala za uzalishaji wa mazao ya kilimo ili kilimo hicho kiwe na tija na pia kiwaongezee kipato chao wenyewe wakulma, jamii zao na mataifa yao kwa ujumla. Miongoni mwa wakulima waliochukua hatua hizo ni Thabo Lefatle ambaye anazalisha mboga za majani akitumia vibanda vya kilimo vinavyozingatia mazingira na katika makala hii Siraj Kalyango anafafanua kwa undani zaidi.

Audio Credit
Siraj Kalyango/Grace Kaneiya
Audio Duration
3'28"
Photo Credit
FAO