Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Marufuku ya matumizi ya plastiki Uganda yasuasua

Marufuku ya matumizi ya plastiki Uganda yasuasua

Pakua

Idadi kubwa ya mifuko ya Plastiki inayotumika katika nchi nyingi duniani husususan nchi zinazoendelea ina madhara kwa ardhi, mito, baharí kutokana na kuwa haiozi. Viumbe vya ardhini na majini huathiriwa na plastiki kwanza kutokana na kemikali zinaounda plastiki hizo au kwa kuwadhuru wanyama au ndege  baada ya kumeza plastiki hizo na wakati mwingine kusababisha vifo. Umoja wa Mataifa unataka sitisho la matumizi ya mifuko hiyo na badala yake kuwepo na mbadala ili kuepusha uharibifu wa siyo tu mazingira bali pia afya za binadamu na viumbe wengine hai. Mataifa mengi yamechukua hatua kadhaa za kukabiliana na plastiki mfano Uganda miaka kadhaa iliyopita ilipiga marufuku utumiaji wa mifuko ya plastiki. Lakini utekelezwaji wa marufuku hiyo ni wa kusuausua. Ni kwa nini? Basi ungana na John Kibego kwa undani wa suala hilo.

Audio Credit
Siraj Kalyango/John Kibego
Audio Duration
4'
Photo Credit
UN Photo/Martine Perret