Ndoto zilizoingia katika mashaka ukimbzini, Uganda.
Vijana ndio nguzo za kufanikisha malengo ya maendeleo endelevu, SDGs, kwani ndio viongozi wa sasa na wa hapo baadaye. Lakini wengi wanakabiliwa na changamoto za kuweza kufanya vitu ambavyo vitawafaa hapo baadaye. Hali ya vijana katika mataifa yanayaoinukia ni ya shida mno. Hii ni kwa kuwa hujikuta ndoto zao za kujiendeleza wakati mwingine zinakwama kabisa na huenda si kwa sababu za kujitakia.
Kijana mmoja kwa jina la Tango Patrick,ni mkimbizi kutoka Jamhuri ya kidemokrasia ya Congoambaye sasa anaishi Uganda na anapenda sana kuimba na mara kwa mara wanaburudisha wakimbizi wenzake , kimuziki ,wakati wa sherehe mbalimbali licha ya changamoto kadhaa kama za kifedha ambazo zinakwamisha ndoto yake ya kuwa mwanamuziki nyota sio tu katika kanda ya Afrika Mashariki na kati lakini pia na duniani kote.
Ili kujua undani wa ndoto ya kijana huyo tuungane na mwandishi wetu wa Uganda John Kibegoambaye alikutana naye katika makaazi ya wakimbizi ya Nakivale magharibi mwa Uganda. Anaanza kwa kumpa kionjo .