Wakimbizi si maadui, ni watu wa kawaida waliokimbia kwao kutokana na taabu- Mariella

13 Julai 2018

Shida inapobisha hodi mara nyingi binadamu hukata tamaa na kuamini kuwa huo ndio mwisho wa maisha  yake. Ingawa hiyo kwa wengine kukata tamaa ni mwiko kwa kuwa wanaamini kuwa mlango mmoja ukifungwa, mingine mingi hufunguka. Hivyo ndivyo ilivyokuwa kwa Mariela Shaker, mkimbizi kutoka Syria ambaye alipo hii leo, katu hakuna mtu ambaye angaliwaza kuwa angaliweza kufika. Vita, mateso, ghasia, ndio yalikuwa mazoea hadi siku ambayo anakwenda kuchukua diploma yake baada ya kuhitimu chuo, kombora likasambaratisha ndoto zote. Hata hivyo baada ya kuamini kuwa ana fursa nyingine alisaka shule na kukubaliwa chuo kimoja kikuu nchini Marekani. Hii leo ni mtumbuizaji wa kutumia fidla huku akitoa simulizi za alikotoka na kutia moyo watu kupitia shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR. Kwa kina basi Flora Nducha anakusimulia.

Audio Credit:
Flora Nducha
Audio Duration:
4'13"

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud