Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Vijana wakishikwa watashikamana kuleta maendeleo katika jamii

Vijana wakishikwa watashikamana kuleta maendeleo katika jamii

Pakua

Vijana ni nguzo muhimu ya kufanikisha ufanisi wa malengo ya maendeleo endelevu au SDGs kwa kuwa wana uwezo na  busara kuweza kuongoza dunia kesho na hata leo. Ili kutimiza hayo vijana hao wanapaswa kuwezeshwa leo kwa kupewa mafunzo yanayohitajika ,ikiwemo kupata elimu ya kutosha, kupata chakula, huduma za afya bora pamoja na malezi mazuri.

Na mtu wa kwanza kuhakikisha hayo kwa kijana ni mzazi , kisha familia na hatimaye jamii. Hata hivyo kwa vijana wengi hili wanaliona kama ndoto kwa sababu ya changamoto lukuki zinazowaandama na kuwakatisha tamaa.

Mathalani wale walioachwa yatima baada ya kupoteza wazazi  au walezi na wao kugeuka kuwa walezi wa wadogo zao au kwa wale wanaoshi na mzazi mmoja ambaye hajiwezi. Matokeo yake kupata elimu inakuwa changamoto sababu ya karo, mlo wao na ndugu zao na hata kodi ya pango ni lazima wakasake.

Siraj Kalyango anamlika binti wa miaka 18 aliyepitia mtihani huu. Ambatana nao katika Makala hii.

Audio Credit
Grace Kaneiya/Siraj Kalyango
Audio Duration
4'
Photo Credit
Alhagie Manka/ UNFPA Gambia