Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tunawapatia vijana stadi za kujikwamua kama kusuka nywele na ushoni- FPMHE

Tunawapatia vijana stadi za kujikwamua kama kusuka nywele na ushoni- FPMHE

Pakua

Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, mashirika ya kiraia yamekuwa yakiunga mkono harakati za kukwamua vijana kutoka katika madhila mbalimbali ikiwemo umaskini. Hatua hiyo inatokana na ukweli kwamba vita nchini humo vimesababisha vijana wa kike na wa kiume kujitumbukiza kwenye mambo yasiyofaa kama vile uasherati, uvutaji wa bangi na hata uporaji. Miongoni mwa mashirika hayo ni FPMHE ambao ni mfuko wa kidugu ulioasisiwa na mchungaji Maurice D’Hoore pamoja na Marceline Tawembi-Njdeka. Bi. Tawembi-Njdeka yuko kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani na amezungumza na Assumpta Massoi kuelezea ni mambo gani yanayofanywa na shirika lake lenye makao makuu kwenye jimbo la Kinshasa ili kukwamua kundi hilo. Anaanza kwa kuelezea kilichochochea yeye kuelekeza usaidizi kwa wasichana.

 

 

Audio Credit
Siraj Kalyango- Assumpta Massoi
Audio Duration
4'5"
Photo Credit
Halima akimhudumia mteja wake wakati wa mafunzo ya kutengeneza nywele anayopata kupitia usaidizi wa PASADA. (Picha:UNICEF/Videocapture)