Wanawake Burundi tumetoka mbali,japo bado kuna changamoto:Nzeyimana
Pakua
Wanawake nchini Burundi wamepiga hatua kubwa katika nyanja mbalimbali ikiwemo masuala ya uongozi baada ya serikali kuwahakikishia uwakilishi wa asilimia 30 bungeni.
Hata hivyo bado kuna changamoto katika kutimiza malengo ya maendeleo endelevu SDG’s yahusuyo wanawake kama usawa wa kijinsia, elimu, haki za kurithi na fursa za kiuchumi hususan wale waishio vijijini.
Katika makala hii mwandishi wetu wa maziwa Makuu Ramadhani KIBUGA ameketi na kuzungumza na mbunge wa Burundi katika bunge la Jumuiya ya Afrika ya Mashariki Leontine Nzeyimana kutathimini hali ya mwanamke nchini humo .
Audio Credit
Siraj Kalyango/Ramadhani Kibuga
Audio Duration
4'27"