Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Makala

Radio Domus: Kevin Keitany

Maji yanaweza kuleta amani au kuchochea migogoro

Ikiwa leo ni Siku ya Kimataifa ya Maji, Kevin Keitany wa redio washirika wetu Domus FM ya nchini Kenya amezungumza na baadhi ya wakazi wa Kaunti ya Kajiado nchini humo kuhusu umuhimu wa uwepo wa maeneo mengi ya kupata maji katika jamii. Dhima ya Siku ya Kimataifa ya Maji ya mwaka huu wa 2024 ni "Maji kwa ajili ya amani" ikieleza kuwa kunapokuwa na ushirikiano katika suala la maji inaleta athari chanya kukuza maelewano, kuhamasisha ustawi na kujenga uwezo wa kukabiliana na changamoto za pamoja. 

Sauti
3'15"
UN News/Ziad Taleb

Watoto Gaza waamua vita isiwe sababu ya kunyong’onyea wakati huu wa mwezi mtukufu wa Ramadhani

Huko Ukanda wa Gaza, vita inayoendelea tangu Oktoba 7 mwaka 2023 baada ya Hamas kurusha makombora Israel na kisha Israel kuamua kujibu mashambulizi licha ya kusababisha vifo vya watu 31,000 wengi wao wakiwa wanawake na watoto, watoto waliosalia wameona mwezi huu Mtukufu wa Ramadhani usipite hivi hivi. Wakiwa katika kambi ya wakimbizi wa ndani ya Deir El Balah katikati mwa Gaza, watoto hao wameona furaha ni bora kuliko machungu ya njaa, ukimbizi, ukosefu wa huduma muhimu za kijamii unaowakabili.

Sauti
4'35"
Credit: UN News/Assumpta Massoi

LANDESA yaelezea ni vipi ushiriki wao CSW68 unaleta nuru kwa wanawake Tanzania

Mkutano wa 68 wa Kamisheni ya Hali ya Wanawake duniani, CSW68 ukiendelea hapa kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa imeendelea kuzungumza na washiriki ili kufahamu yale wanayofanya kutekeleza maudhui ya kipaumbele ya mwaka huu ya kumwezesha mwanamke na mtoto wa kike ili hatimaye kupunguza umaskini na kuimarisha usawa wa kijinsia. Shirika la kiraia la kutetea haki ya ardhi kwa wanawake, LENDESA tawi la Tanzania linaloungwa mkono na shirika la Umoja wa Mataifa la kushughulikia masuala ya wanawake ni miongoni mwa washiriki  ambapo Assump

Sauti
5'18"
UNIS/Stella Vuzo

Mlo shuleni umeongeza idadi ya wanafunzi wangu shule ya Salama: Mwalimu Beatrice Osaka

Shule ya Salama iliyo katika eneo la Huruma karibu na mtaa wa mabanda wa Mathare jijini Nairobi Kenya hivi karibuni imeanza programu ya mlo shuleni kupitia mradi wa kampuni ya ‘Food for Education”. Hatua hiyo imenfa idadi ya wanafunzi wanaosoma shule hiyo kuongezeka kutoka 1, 900 hadi 2,300. Mlo shuleni ni moja ya masuala ambayo yanapigiwa debe kubwa na Umoja wa Mataifa sio tu kwa sababu ya kuhakikisha lishe bora kwa mamia ya maelfu ya wanafunzi ambao wengi hawawezi kupata mlo nyumbani bali pia kuongeza idadi ya watoto wanaohudhuria masomo.

Sauti
5'8"
Habari za UN

KIGOMa: Mafunzo ya kilimo hifadhi kutoka FAO chaongeza mavuno mahindi kutoka magunia 4 hadi 45

Sasa ni makala inayotupeleka mkoani Kigoma, kaskazini-magharibi mwa Tanzania ambako huko shirika la Umoja wa Mataifa la chakula na kilimo, FAO limetekeleza kwa vitendo ujumbe wa mwaka huu wa siku ya wanawake duniani, Wekeza kwa Wanawake, Songesha Maendeleo, kwa kuwapatia mafunzo ya ufugaji bora wa kuku na mbuzi, halikadhalika kilimo hifadhi kisichoharibu mazingira. Sasa manufaa yako dhahiri kwani wanawake wameinuka kiuchumi. Miongoni mwao ni Hadija Alisido, mkazi wa kijiji Muhange, wilaya ya Kakonko.

Sauti
3'50"
UN News

Wanawake na wasichana wakiwezeshwa jamii zinanufaika - Wanabiashara Kenya

Wiki hii Ijumaa tarehe 8 Machi 2024, ulimwengu utaadhimisha Siku ya Wanawake Duniani ambapo mwaka huu ina maudhui “Wekeza kwa wanawake: Harakisha maendeleo,” lakini Shirika la Umoja wa Mataifa la masuala ya wanawake, UN Women linasema ni dhahiri kwamba ulimwengu bado unakabiliwa na migogoro mingi, kuanzia mizozo ya kijiografia hadi viwango vya umaskini vinavyoongezeka, ukosefu wa usawa na kuongezeka kwa athari za mabadiliko ya tabianchi.

Sauti
4'19"