Makala

Mradi wa UN na Tanzania wapeleka furaha kwa wanakijiji wa Magunga mkoani Tanga

Mwezi  uliopita wa Oktoba, wakazi wa kijiji cha Magunda, wilaya  ya Korogwe mkoani Tanga nchini Tanzania waligubikwa na furaha isiyo kifani baada ya kushuhudia mashamba yao yakigeuka kuwa kitegauchumi na mtaji kwa ajili ya kuboresha maisha yao.

Sauti -
4'16"

Tukifanikiwa kuondoa pengo kati ya wanawake na wanaume tutakuwa na jamii endelevu-Kijana Koka

Suala la ajira kwa vijana ni changamoto katika nchi nyingi na sasa hivi kuna wito wa kubadili hali ambapo vijana wenyewe wamechukua jukumu la kujiajiri wenyewe au kufanya kazi za kujitolea.

Sauti -
5'44"

Mtazamo wa wazee kwa ndoa za utotoni huko Turkana

Ndoa za mapema ni jinamizi lililojikita mizizi katika tamaduni mbalimbali hasa zile za wafugaji barani Afrika, zikiathiri vibaya ustawi wa watoto wa kike.

Sauti -
3'57"

Kauli ya wahenga kuhusu samaki ni dhahiri kwa Wanjuhi Njoroge

Wahenga walinena kuwa samaki mkunje angali mbichi kwani akikauka hakunjiki! Hivyo ndivyo ilivyokuwa kwa mwanaharakati wa mazingira nchini Kenya, Wanjuhi Njoroge ambaye hivi sasa suala la miti na mazingira ni jambo ambalo ni sawa na kusema linatiririka kwenye damu ya mwili wake.

Sauti -
4'20"

Uvumbuzi wa mashine ya kukausha nafaka ni habari njema kwa mkulima Thika, Kenya

Wakulima wengi hukumbwa na changamoto za kuhifadhi mazao yao baada ya kuyavuna hususan nafaka hali inayawaletea hasara kubwa ya kupoteza chakula na hali kadhalika kusababishia familia zao taabu kama vile ukosefu wa chakula.

Sauti -
2'53"

Tukiwainua walezi, tunaiinua familia nzima-Mary Mafwimbo

Na punde ni makala ambapo leo tunaelekea Tanzania kusikia harakati za msichana ambaye ameanzisha ‘shirika la kiraia la kuhudumia wanawake, wazee na watoto huko mkoani Morogoro.

Sauti -
3'7"

Jinamizi la ndoa za mapema katika jamii ya wafugaji wa Kiturkana, Kenya

Ndoa za mapema ni jinamizi kubwa lilalowandama watoto wa kike hasa katika jamii za wafugaji duniani kote, kutokana na tabia ya kulinganisha mtoto wa kike na maelfu ya mifugo.

Sauti -
3'43"

IFAD yarejesha matumaini ya wakulima wa milimani Morocco

Nchini Morocco mradi unaofadhiliwa na mfuko wa maendeleo ya kilimo wa Umoja wa Mataifa, IFAD umeendelea kuwa na mafanikio makubwa hususan kwa wanufaika ambao ni wakazi wa milimani. Mradi huo ulioanza mwaka 2011 na unatamatishwa mwaka huu wa 2019  unalenga watu 33,000 wengi wao wakiwa ni wakulima

Sauti -
3'

Wakimbizi wakaribisha mradi wa WFP kuimarisha “lishe”, Uganda

Jamii za wakimbizi kote duniani hukabiliwa na changamoto za upatikanaji wa lishe na uhakika wa chakula kutokana na ukata wa ufadhili na kutokuwa na ardhi ya kutosha ili kujishughulisha na kilimo.

Sauti -
3'45"

Ubunifu wa spika janja Kaya sasa kuanza kuingia sokoni mwakani

Kila uchao Umoja wa Mataifa unapigia chepuo ushiriki wa vijana katika kuleta mabadiliko katika dunia ya sasa na kuhakikisha mustakabali wa kizazi kijacho unakuwa bora.

Sauti -
4'26"