Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Jarida la Habari

27 SEPTEMBA 2023

Hii leo jaridani tuanaangazia usafirishaji baharini, na ulinzi wa amani. Makala tunakupeleka mjini Roma na mashinani tutasalia hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa, kuikoni?

Sauti
9'56"
UN News/Jing Zhang

UNCTAD: Hatua za kijasiri zahitajika kukabili hewa ya ukaa kwenye usafiri baharini

Usafirishaji baharini unapaswa kuangaliwa upya ili kupunguza hewa ya ukaa au kaboni inayochafua mazingira, imesema ripoti mpya iliyotolewa leo na Kamati ya Umoja wa Mataifa ya Maendeleo ya Biashara duniani, UNCTAD. 

Ikipatiwa jina Usafiri wa Baharini mwaka 2030, ripoti inahimiza hatua za kijasiri na ushirikiano wa mfumo mzima kwa kuzingatia umuhimu wake duniani lakini vile vile uchafuzi wake wa mazingira sababu kuu ikiwa vyombo hivyo vya usafiri maji kuwa kuukuu.  

Mkurugenzi wa UNCTAD anayehusika na teknolojia Shamika N. Sirimanne anasema, 

Sauti
2'3"

26 SEPTEMBA 2023

Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina ambapo hivi karibuni Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC Félix-Antoine Tshisekedi Tshilombo alihutubia mjadala mkuu wa mkutano wa 78 wa Baraza  Kuu la Umoja wa Mataifa na kutangaza kuwa uchaguzi mkuu uliopangwa kufanyika nchini humo mwishoni mwa mwaka huu, utafanyika kama ilivyopangwa. Alisema tayari Tume Huru ya Uchaguzi nchini DRC, CENI [SENI] imeshachapisha majina ya wagombea na michakato mingine inaendelea.

Sauti
11'49"

25 SEPTEMBA 2023

Hii leo jaridani tunaangazia machafuko nchini Ukraine na mkutano wa kimataifa huko Rome kuhusu marekebisho ya mfumo wa ufugaji wa wanyama. Makala tunasalia hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa na mashinani tunakupeleka nchini Poland, kulikoni?

Sauti
12'56"

21 SEPTEMBA 2023

Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina ambapo wiki hii hapa kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa kumefanyika mkutano wa tathmini ya malengo ya maendeleo endelevu SDGs kuona wapi nchi wanachama, kampuni, watu binafsi wamefikia kusongesha maendeleo hayo yanayofikia ukomo mwka 2030. Vijana nao walikuwa na siku zao mbili za kuelezea wanafanya nini kule waliko na wanataka nini kifanyike kusongesha malengo hayo likiwemo namba 13 la tabianchi.

Sauti
12'28"

20 SEPTEMBA 2023

Hii leo jaridani tunakuletea maoni kuhusu matumizi ya lugha ya kiswahili kutokwa kwa viongozi wanaoshiriki UNGA78, na yaliyojiri hapa makao makuu katika mjadala kuhusu malengo ya maendeleo endelevu. Makala tunakupeleka nchini Kenya na mashinani tunasalia hapa makao makuu, kulikoni?  

Sauti
14'56"

19 SEPTEMBA 2023

Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina ambapo Leo ni siku ya pili na ya mwisho wa mkutano kuhusu malengo ya maendeleo endelevu SDGs lakini leo pia ndio pazia la mjadala Mkuu wa 78, UNGA78 limefunguliwa na pamoja na na hotuba za viongozi pia kutakuwa na mikutano itakayo jadili hali za ulinzi na usalama katika mataifa mbalimbali na hapo kesho kutakuwa na mkutano wa ngazi ya juu kuhusu Sudan. Pia tunakuletea habari kwa ufupi na nashinani ikimulika hotuba za viongozi katika Baraza Kuu na kazi za vijana katika utekelezaji wa DGs.  

Sauti
11'34"