Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

25 SEPTEMBA 2023

25 SEPTEMBA 2023

Pakua

Hii leo jaridani tunaangazia machafuko nchini Ukraine na mkutano wa kimataifa huko Rome kuhusu marekebisho ya mfumo wa ufugaji wa wanyama. Makala tunasalia hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa na mashinani tunakupeleka nchini Poland, kulikoni?

  1. Tume ya Umoja wa Mataifa ya Uchunguzi kuhusu Ukraine imeripoti leo kwa Baraza la Haki za Kibinadamu kwamba kuna ushahidi unaoendelea kuwa wanajeshi wa Urusi wanafanya uhalifu wa kivita nchini Ukraine.
  2. Mkutano wa kwanza kabisa wa kimataifa kuhusu marekebisho ya mfumo wa ufugaji wa Wanyama umeanza hii leo kwenye makao makuu ya shirika la Umoja wa Mataifa la chakula na kilimo, FAO lengo likiwa ni kusaka mbinu za kuwezesha ufugaji huo uwe na mnepo zaidi, usiharibu mazingira na uchangie katika maendeleo endelevu ya kiuchumi na kijamii, halikadhalika sayari yenye afya.
  3. Katika makala Waziri wa Afya wa Tanzania Ummy Mwalimu aliketi chini na Flora Nducha wa Idhaa hii ya Kiswahili kuzungumzia mikakati ya nchi hiyo katika kulitekeleza azimio la Umoja wa Mataifa la kuchukua hatua kuhusu huduma za afya kwa wote ifikapo mwaka 2030.
  4. Mashinani tunakupeleka nchini Poland kusikia jinsi ambavyo wakimbizi wa Ukraine walivyoshindwa kuendelea na matibabu ya kifua kikuu baada ya kulazimika kukimbia makwao.

Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!

Audio Credit
Leah Mushi
Audio Duration
12'56"