Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

29 SEPTEMBA 2023

29 SEPTEMBA 2023

Pakua

Hii leo jaridani tunaangazia utupaji wa chakula, na uchaguzi ujao nchini Sudan Kusini. Makala tunakupeleka nchini Uganda na mashinani nchini DRC, kulikoni?.

  1. Hii leo kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa New York, Marekani, Baraza la Usalama limejadili hali ya kibinadamu nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC ambapo awali Naibu Mkuu wa ofisi ya Umoja huo kuhusu misaada ya kiutu Joyce Msuya anataja changamoto zinazokumba taifa hilo.
  2. Wakati nchi ya Sudan Kusini ikijiandaa kushiriki katika uchaguzi mkuu kwa mara ya kwanza kabisa tangu ipate uhuru, Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo UNMISS unaendesha makongamano na vyama vya siasa nchini humo.
  3. Makala inatupeleka nchini Uganda kumsikiliza Gad Harindimana, kijana mkimbizi kutoka Rwanda anayeishi katika makazi ya wakimbizi Nakivale mnufaika wa programu ya Huduma za Ajira Vijijini inayoungwa mkono na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kazi Duniani, ILO kupitia shirika lisilo la kiserikali la AVSI Foundation. Harindimana anasimulia kwa lugha ya Kinyakole inayotafsiriwa na Anold Kayanda.
  4. Katika mashinani tutammsikia mwanamke ambaye aliweza kujifungua salama, na bila malipo, kwa usaidizi wa wakunga katika kliniki tembezi inayohifadhiwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya ya Uzazi na Idadi ya watu, UNFPA katika kambi ya wakimbizi wa ndani mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, DRC.

Mwenyeji wako ni Assumpta, karibu!

Audio Credit
Assumpta Massoi
Sauti
12'8"