Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

27 SEPTEMBA 2023

27 SEPTEMBA 2023

Pakua

Hii leo jaridani tuanaangazia usafirishaji baharini, na ulinzi wa amani. Makala tunakupeleka mjini Roma na mashinani tutasalia hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa, kuikoni?

  1. Usafirishaji baharini unapaswa kuangaliwa upya ili kupunguza hewa ya ukaa au kaboni inayochafua mazingira, imesema ripoti mpya iliyotolewa leo na Kamati ya Umoja wa Mataifa ya Maendeleo ya Biashara duniani, UNCTAD.
  2. Mkuu wa Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR, MINUSCA, Jenerali Humphrey Nyone amewataka walinda amani kutoka Tanzania wanaohudumu nchini humo chini ya MINUSCA kuendelea na moyo wa uchapa kazi huku wakizingatia kuepuka unyanyasaji na unyonyaji wa kingono.
  3. Katika makala Evarist Mapesa anayetuletea makala kutoka nchini Thailand ikiangazia mradi unaotekelezwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la chakula na kilimo FAO wakusaidia wafanyabiashara kupunguza upotevu na utupaji wa chakula.
  4. Mashinani tunasalia katika ajenda 2030 ya malengo ya maendeleo endelevu kusikia ujumbe wa Orlando Bloom, Balozi Mwema wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto, UNICEF.

Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!

Audio Credit
Assumpta Massoi
Audio Duration
9'56"