Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

22 SEPTEMBA 2023

22 SEPTEMBA 2023

Pakua

Hii leo jaridani tunaangazi ugonjwa wa kifua kikuu na haki za wanawake nchini Iran. Makala na mashinani tunasalia hapa hapa makao makuu wa Umoja wa Mataifa, kulikoni?

  1. Mkutano wa ngazi ya juu wa Umoja wa Mataifa kuhusu mapambano dhidi ya Kifua Kikuu au TB ukifanyika leo hapa katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York Marekani, Waziri wa Afya wa Kenya Susan Nakhumicha Wafula amesema kutokomeza TB ifikapo mwaka 2030 inawezekana endapo dunia itashikamana na kuweka msokumo mkubwa kwa ugonjwa huo kama ilivyofanya wakati wa mlipuko wa janga la COVID-19.
  2. Hatua ya Bunge la Iran kupitisha mswada mpya utakaowabana zaidi wanawake kuhusu uhuru wa miili yao na pia uvaaji wao hususani vazi la Hijab imepokelewa kwa masikitiko makubwa  na Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya haki za binadamu, OHCHR.
  3. Katika makala hii leo hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa kunafanyika mkutano wa pili wa ngazi ya juu kutathmini azimio la kisiasa la mwaka 2018 kuhusu kutokomeza ugonjwa wa Kifua Kikuu ifikapo mwaka 2030. Evarist Mapesa wa Idhaa hii amezungumza na Dokta Abdallah Keresa kutoka kitengo cha Kliniki ya Kifua Kikuu na Virusi vya Ukimwi (VVU) Hospitali ya Rufaa ya Bugando mkoani Mwanza nchini Tanzania ambapo pamoja na kueleza mafanikio ya kudhibiti TB, anaanza kwa kueleza umhimu wa mkutano huu.
  4. Mashinani tutasalia hapa Makao Makuu kupata ujumbe wa Rais wa Guinea kwa viongozi wa Dunia.

Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!

Audio Credit
Assumpta Massoi
Audio Duration
12'31"