Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

22 NOVEMBA 2022

22 NOVEMBA 2022

Pakua

Hii leo jarida linaangazia Mada kwa kina tukimulika kongamano la kimataifa la wataalam wa kifua kikuu au TB lmjini Nairobi, Kenya na habari kwa ufupi ikiangazia kazi za Umoja wa Mataifa nchini Morocco, maandamano nchini Iran na walinda amani wa Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC.  Na mashinani tutaelekea Visiwa vya Solomoni katika eneo la kusini mwa Bahari ya Pasifiki, huko msemo wa "Majuto Mjukuu" umekuwa dhahiri,  kulikoni?

  1. Kifua kikuu husambazwa kupitia hewa pale mtu anapovuta iliyo na bakteria aina ya Mycobacterium tuberculosis wakati wa kukohoa. Kwa mujibi wa shirika la afya la Umoja wa Mataifa duniani WHO, TB ni moja ya magonjwa 10 yanayosababisha vifo vingi duniani. kwa kiasi kikubwa kifua kikuu huathiri mapafu lakini sehemu nyengine mwilini pia zinaweza kuambukizwa. 
  2. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amehutubia jukwaa la ustaarabu huko Morocco na kusema changamoto zote zinazokumba dunia kuanzia amani na usalama ,maendeleo na mabadiliko ya tabianchi nchi zinafahamika, halikadhalika majawabu yake lakini jambo ambalo bado lina utata ni kwa vipi majawabu hayo yatatekelezwa, na ndipo akasema jukwaa hilo linalochagiza stahmala na kuishi pamoja kwa amani ndio nuru ya sasa.
  3. Kutoka Geneva, Uswisi, Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za binadamu, Volker Turk amesema ongezeko la vifo vya watu kutokana na maandamano nchini Iran wakiwemo watoto wawili waliofariki mwishoni mwa wiki pamoja na msimamo mkali wa vikosi vya usalama kunatia shaka kuhusu hali ya usalama nchini humo.
  4. Na Kamanda Mkuu wa vikosi vya Umoja wa Mataifa vya ujumbe wa kulinda amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, MONUSCO Luteni Jenerali Marcos De Sá Affonso Da Costa amepongeza hatua za walinda amani kutoka Afrika Kusini kwenye ujumbe huo za kusafirisha wanajeshi majeruhi wa jeshi la DRC, FARDC waliojeruhiwa wakati wa mapigano kati yao a waasi wa kikundi cha M23 huko Kivu Kaskazini.
  5. Na leo mashinani tutaelekea katika Visiwa vya Solomoni katika eneo la kusini mwa Bahari ya Pasifiki kusikia majuto ya mwanaume mmoja anayejutia kutekeleza unyanyasaji wa kijinsia.

Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!

Audio Credit
Assumpta Massoi
Sauti
12'5"