Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

28 NOVEMBA 2022

28 NOVEMBA 2022

Pakua

Hii leo jarida linakuletea habari za WHO na michuano ya fainali za Kombe la Dunia. Makala inatupeleka kambi ya wakimbizi ya Kakuma nchini Kenya kusikia simulizi ya msichana mnufaika wa mradi wa Girl Shine na Mashinani tutaelekea nchini Uganda kwa mkimbizi mwanaharakati wa mazingira

  1. Baada ya mfululizo wa mashauriano na wataalamu wa kimataifa, hatimaye shirika la Umoja wa Mataifa la afya ulimwenguni, WHO litaanza kutumia jina MPOX badala ya Monkeypox au homa ya Ndui ya Nyani kufuatia mapendekezo ya kubadilishwa kwa jina hilo kwa maelezo ya kwamba lilikuwa linasababisha mambo kadhaa ikiwemo unyanyapaa.
  2. Michuano ya fainali za Kombe la Dunia kwa mchezo wa soka kwa wanaume inaendelea nchini Qatar huko Mashariki ya Kati. Mmoja wa watu wanaong’ara katika michuano hii ni Mchechemuzi wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF Rwanda, Salima Mukansanga, ambaye ameweka historia ya kuwa mwanamke wa kwanza mweusi kuwa mwamuzi au refarii katika Kombe la Dunia.
  3. Makala inatupeleka kambi ya wakimbizi ya Kakuma nchini Kenya kusikia simulizi ya msichana mnufaika wa mradi wa Girl Shine, unaolenga kupatia wasichana barubaru stadi za kiuchumi, uongozi na msaada wa kisaikolojia ili waweze kujikwamua na kujitambua katika mazingira hatarishi waliyomo.
  4. Na leo mashinani tutaelekea nchini Uganda kwa mkimbizi mwanaharakati wa mazingira

Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!

Audio Duration
10'56"