Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

25 NOVENBA 2022

25 NOVENBA 2022

Pakua

Hii leo jarida linaangazia afya nchini Haiti na ujenzi wa amani hasa kwa lengo la kuepusha vijana kutumbukizwa kwenye vikundi vyenye msimamo mkali huko Garissa nchini Kenya. Makala tunakwenda nchini Poland na Mashinani nchini Ethiopia, kuliko ni?  

  1. Ikikaribia miezi miwili tangu kuzuka kwa mlipuko wa kipindupindu nchini Haiti shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF limeonya kwamba takriban asilimia 40 ya ongezeko la idadi ya wagonjwa ni watoto na hatua zaidi zinahitajika ili kuwanusuru.
  2. Nchini Kenya shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya wanawake, UN Women kwa ushirikiano na wadau wanajengea uwezo wajenzi wa amani mashinani hata kwenye maeneo yenye changamoto kama vile kambi ya wakimbizi ya Daadab kwenye kaunti ya Garissa nchini humo kwa lengo la kuepusha vijana kutumbukizwa kwenye vikundi vyenye msimamo mkali.
  3. Makala tunaelekea barani Ulaya, nchini Poland katika mji wa Libiąż kusikia harakati za Benki ya Dunia kwa kushirikiana na serikali za mtaa, makundi ya kijamii, vyama vya wafanyakazi na kijamii kuondokana na nishati ya makaa ya mawe ambayo ni hatari kwa mazingira na sayari dunia kwa ujumla.
  4. Na leo mashinani tunakwenda nchini Ethiopia ambako huko tunamulika juhudi za Umoja wa Mataifa kutokomeza aina zote za ukatili dhidi ya wanawake na mtoto wa kike.

Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!

Audio Credit
Assumpta Massoi
Audio Duration
10'28"