Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

23 NOVEMBA 2022

23 NOVEMBA 2022

Pakua

Hii leo jarida linamulika ukatili dhidi ya wanawake na wasichana na pia mradi wa kupatia fedha jamii nchini Malawi. Makala tunakwenda nchini Kenya na Mashinani nchini Tanzania.

  1. Ripoti ya utafiti mpya iliyotolewa leo na shirika la Umoja wa Mataifa la masuala ya wanawake UN Women na ofisi ya Umoja wa Mataifa ya madawa na uhalifu UNODC inaonyesha kuwa wanawake na wasichana ndio walio katika hatari kubwa ya kuuawa majumbani, ikionyesha kuwa kwa wastani zaidi ya wanawake au wasichana watano waliuawa kila saa na wenzi wao au jamaa wa familia kwa mwaka 2021. Flora Nducha na taarifa zaidi
  2. Nchini Malawi,shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto duniani, UNICEF kwa msaada kutoka kwa wadau wake wa maendeleo linatekeleza mradi wa kupatia fedha jamii au MSCTP kwa ajili ya kupunguza umaskini, kukabili utapiamlo halikadhalika kuondokana na utoro shuleni utokanao na wazazi kushindwa kulipa karo.
  3. Makala ambapo tunaelekea nchini Kenya katika Kaunti ya Garissa kuangazia hali mbaya ya ukame iliyosababishwa na mabadiliko ya tabianchi na hatua zinazochukuliwa na Umoja wa Mataifa kwa kushirikiana na serikali.
  4. Na leo mashinani na tunakwenda nchini Tanzania kusikia ni harakati za kunusuru wanawake dhidi ya ukatili kwa misingi ya umiliki wa ardhi.

Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!

Audio Credit
Assumpta Massoi
Audio Duration
14'25"