Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

30 NOVEMBA 2022

30 NOVEMBA 2022

Pakua

Jaridani leo tunaangazia mtandao wa intaneti barani Africa na juhudi za UNICEF Uganda katika shule moja ya msingi nchini humo. Makala tutaelekea nchini Tanzania Kusini Magharibi katika mkoa wa Mbeya na mashinani tutasalia hukohuko nchini Tanzania katika kambi ya wakambizi ya Nyarugusu.

  1. Nchi za Afrika zimechagizwa kuwekeza katika kujenga mnepo wa miundombinu thabiti ya ya mtandao wa intaneti ili kutumia fursa za kidijitali na kuharakisha mageuzi ya kijamii na kiuchumi barani humo.
  2. Nchini Uganda shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF limewezesha wanafunzi wa shule moja ya msingi nchini humo kufanya mtihani wa kuhitimu shule ya msingi baada ya shule hiyo kulazimika kufungwa na wanafunzi kuwekwa karantini kufuatia mwanafunzi mmoja kupata maambukizi ya Ebola, mlipuko uliotangazwa mwezi Septemba mwaka huu. 
  3. Makala tutaelekea nchini Tanzania Kusini Magharibi katika mkoa wa mbeya kusikia wananchi wa wilaya ya Rungwe wanaelewa nini kuhusu Ukatili wa kijinsia wakati huu dunia ikiwa katika siku 16 za kupinga ukatili huo miongoni mwa jamii.
  4. Na mashinani tutasalia hukohuko nchini Tanzania katika kambi ya wakambizi ya Nyarugusu, kulikoni?

Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!

Audio Duration
12'18"