17 Mei 2022

17 Mei 2022

Pakua

Jaridani na Leah Mushi-

HABARI KWA UFUPI 

Idadi ya watoto walioathirika na uzito mdogo wa kupindukia imekuwa ikiongezeka hata kabla ya viya ya Ukraine ambayo inatishia kuitumbukiza dunia kwenye mgogoro mkubwa wa chakula imeonya ripoti mpya kuhusu watoto iliyotolewa leo na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF

==============================================================================================

Mkutano wa 9 wa miji barani Afrika umeanza leo katika mji wa Kisumu nchini Kenya kwa lengo la kuchagiza umuhimu na jukumu la miji ya ukubwa wa kati barani humo.  

Mkutano huo wa siku tano unaofanyika kila baada ya miaka 3 kwenye miji tofauti Afrika umeandaliwa kwa ushirikiano wa shirika la makazi la Umoja wa Mataifa UN-HABITAT, serikali ya Kenya, baraza la magavana Kenya na kaunti ya Kisumu. 

====================================================================================== 

NA shirika la Umoja wa Mataifa la  Chakula na Kilimo FAO kupitia mradi wake wa FISH4ACP limefanya mkutano wa pili wa Kikosi Kazi cha Taifa cha kukuza mnyororo wa thamani wa mazao ya uvuvi katika Ziwa Tanganyika mkoani Kigoma lengo likiwa ni kuimarisha na kujenga mazingira rafiki kwa wanawake ili kufanya shughuli zao katika nyanja ya uchakataji, wafanyabiashara na usafirishaji na kuongeza kipato binafsi na pato la Taifa. 

Katika mada kwa kina tunaangazia namna Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa kusaidia walionyanyaswa kijinsia na kingono ulivyowakwamua wanawake huko Kivu Kusini nchini DRC

Na mashinani tutasikia kutoka kwa mtaalamu kuhusu namna ya kuhakisha kinga dhidi ya Covid-19 kwa watoto hata wakati wakihudhuria shule ana kwa ana.

Audio Credit
Leah Mushi
Audio Duration
12'6"