Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

18 Novemba 2021

18 Novemba 2021

Pakua

Hujambo na karibu kusikiliza jarida ambapo miongoni mwa ukayosikia leo ni pamoja na;- 

Kura ya maoni iliyoendeshwa katika nchi 21 ikihusisha watoto na watu wazima zaidi ya 21,000 imeonesha kuwa watoto wanaamini dunia inakuwa bora zaidi huku watu wazima wakiwa na shaka na shuku.

Mradi wa WFP kwa wakulima Zambia umekuwa neema Mkulima Mainner na familia yake.

Mbali na jukumu la ulinzi wa amani nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati CAR, kikosi cha ulinzi wa amani kutoka Tanzania TANBAT 4 kinachohudumu chini ya mpango wa Umoja wa Mataifa ujulikanao kama MINUSCA nchini humo , kimeweka mikakati ya kusaidia na kuinua wananchi  wa CAR kielimu kupitia shughuli mbalimbali.  

Pia kutoka Goma nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC itasikia kisanga cha watoto waliopotea baada ya mlipuko wa volkano ya mlima Nyiragongo jimboni Kivu Kaskazini na hatimaye wamekutana na mama yao.

Audio Credit
Assumpta Massoi
Audio Duration
11'23"