16 Novemba 2021

16 Novemba 2021

Pakua

Karibu kusikiliza jarida ambapo leo Assumpta Massoi anakuletea habari mbalimbali ikiwemo mgogoro wa wananchi huko Cameroon baada ya kubuni mbinu za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.

Ripoti mpya iliyotolewa leo na shirika la afya la Umoja wa Mataifa inaonyesha kwamba idadi ya watumiaji wa bidhaa za tumbaku duniani imepungua kwa zaidi ya watu milioni mbili.

 Na shirika la Umoja wa Mataifa la kufanikisha upatikanaji wa dawa za tiba kwa gharama,  nafuu, UNITAID, leo limetangaza makubaliano ya kuwezesha dawa ya kutibu ugonjwa wa Corona, COVID-19 kutoka kampuni ya Pfizer ipatikane kwa gharama nafuu kwa nchi za kipato cha chini na kati.

Audio Credit
Assumpta Massoi
Audio Duration
13'11"