Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

23 Novemba 2021

23 Novemba 2021

Pakua

Karibu kusikiliza jarida linaloletwa kwako na Flora Nducha ambapo hii leo nisiku ya furaha kwa wazungumzaji wa wa lugha ya Kiswahili kwani Umoja wa Mataifa umetangaza rasmi Julai 7 kila mwaka kuwa siku ya Kiswahili duniani.

Kutokea nchini Kenya utakutana na Angela Andia mshindi wa mwaka 2021 wa mradi wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF uitwao “wisdom project” au mradi wa busara ambao unashirikisha watoto wa umri wa kati ya miaka 9-14 kila mwaka wakishindana katika kuandaa Habari zinazohusua haki za mtoto.

Na huko nchini Sudan utasikia madhila yanayowakumba wananchi waishio White Nile baada ya kutokea mafuriko ambayo wanasema hawajawahi kuona.

Audio Credit
Flora nducha
Audio Duration
12'15"