Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

27 Julai 2021

27 Julai 2021

Pakua

Hii leo jaridani Assumpta Massoi anaanzia Roma nchini Italia kunakofanyika mkutano tangulizi wa viongozi kuhusu mifumo ya chakula duniani, kisha anakwenda Sudan Kusini ambako huko walinda amani wa Umoja wa Mataifa kutoka Thailand wanatekeleza kauli ya wahenga kuwa mfundishe mtu kuvua samaki badala ya kumpa samaki mmoja. Anasalia huko huko Sudan Kusini akimulika adha ya wakimbizi wa ndani waliofurushwa Tambura jimboni Equatoria Magharibi. Makala ni kuhusu wakimbizi wa ndani nchini Uganda na wito wao kwa serikali kuwapatia eneo la kuishi. Mashinani ni tunarejea nchini Sudan Kusini ambako mshiriki wa warsha anasema kile kinachohitajika kwa ajili ya amani ya kudumu Sudan Kusini.

Audio Credit
Assumpta Massoi
Audio Duration
13'24"